NYOTA wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo sasa
ni kati ya wanamichezo wanne wanaoongoza kwa kuingiza fedha duniani, wakizidiwa
tu mwanamuziki Taylor Swift, Boyband One Direction na James Patterson.
Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa za
jarida la Forbes ambalo limesema mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 31 anaingiza kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 88 kwa msimu.
Kiasi hicho kinamuweka juu ya mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Barcelona anayeingiza dola Milioni 81.5 katika nafasi ya pili na nyota wa timu ya mpira wa kikapu ya Cleveland Cavaliers, LeBron James anayeingiza dola Milioni 77 katika nafasi ya tatu.
Orodha kamili ya wanamichezo 10
wanaoongozwa kulipwa kwa mujibu
Namba
|
Muhusika
|
Pato
lake
|
1.
|
Taylor
Swift
|
Dola
Milioni 170
|
2.
|
One
Direction
|
Dola
Milioni 110
|
3.
|
James
Patterson
|
Dola
Milioni 95
|
=4.
|
Cristiano
Ronaldo
|
Dola Milioni 88
|
=4.
|
Dr.
Phil McGraw
|
Dola
Milioni 88
|
6.
|
Kevin
Hart
|
Dola Milioni 87.5
|
7.
|
Howard
Stern
|
Dola
Milioni 85
|
8.
|
Lionel
Messi
|
Dola Milioni 81.5
|
9.
|
Adele
|
Dola
Milioni 80.5
|
10.
|
Rush
Limbaugh
|
Dola Milioni 79
|
Wanamichezo 10 wanaolipwa zaidi kwa mujibu wa Forbes
|
Kwa mujibu wa Forbes, Ronaldo
anapata Dola Milioni 55 kutokana na mshahara tu, wakati fedha nyingine
zinatokana na mikataba yake ya udhamini.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United anafanya kazi na makampuni ya Nike, TAG Heuer, Sacoor Brothers Suits na Monster.
Si ajabu Mreno huyo kuongoza sasa
kwa kipato hivi sasa, ikiwa hata uwanjani ameendelea kufanya vizuri na mwaka
huu ukiingia katika moja ya miaka ya kukumb ukwa kwenye maisha yake ya soka.
Huu
ni mwaka wa kukumbukwa kwa Cristiano Ronaldo
Mei mwaka huu alifunga penalti ya
ushindi dhidi ya mahasimu wao wa Jiji, Atletico Madrid katika fainali ya Ligi
ya Mabingwa Ulaya kabla ya wiki iliyopita kuiongoza Ureno kutwaa taji la Euro
2016 wakiwafunga wenyeji Ufaransa 1-0 katika fainali.
No comments:
Post a Comment