Umoja wa
madhehebu ya kikristo na kiislamu
Interface Mkoani Geita, imeupongeza mgodi
wa dhahabu wa GGM, kwa
juhudi ambazo umekuwa ukizifanya
za kuhakikisha kwamba wananchi
wananufaika kutokana na uwepo
wa mgodi huo.
Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea
kalakana ya ufundi iliyopo eneo la
magogo kata ya Bomba mbili walipokuwa
wamekwenda kutembelea eneo hilo
kwa lengo la kuona shughuli zinazofanywa
na kalakana hiyo.
Mratibu wa Interface mchungaji John Marko Ndaruka amesema kuwa wameendelea kufaidika na GGM kutokana na
huduma ambazo kwa sasa zinaonekana kwani hapo awali huduma hizo zilikuwa hazifahamiki hivyo
wananchi wengi walikuwa hawaoni faida ya uwepo wa mgodi huo.
Kwa upande wake, shekhe Alhad Yusufu
Kabaju ambae ni mwenyekiti mwenza
wa taasisi hiyo ameongeza kuwa kumekuwepo na maneno kwa jamii
kuwaona kwamba hakuna jambo lolote linalofanywa na GGM, kwani sababu kuu ni
kutokana na viongozi wa serikali kutokuelezwa kazi ambazo zinafanywa na
mgodi katika kuleta maendeleo.
Meneja Mahusiano wa Mgodi wa dhahabu Manase Ndoloma ameeleza
kuwa thamani ya miradi inaweza kufikisha
Dola milioni moja endapo kila kitu kitakuwa kimekamilika katika kalakana hiyo.
No comments:
Post a Comment