Mwakilishi wa Shirika la Watoto Duniani(UNICEF)
Bi.Cecilia Baldeh akieleza jambo wakati wa uzinduzi wa matokeo ya utafiti wa
utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara uliofanyika katika ukumbi
wa Wizara ya Fedha na Mipango leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt
Albina Chuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu ripoti ya matokeo utafiti wa
utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara uliofanyika katika ukumbi
wa Wizara ya Fedha na Mipango leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira
na Walemavu Dk. Abdallah Possi akizungumza kabla hajazindua matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto
wa mwaka 2014 Tanzania Bara uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango
leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Dk. Abdallah Possi akionyesha ripoti
ya matokeo ya utafiti wa utumikishwaji
wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara mara baada ya kuizindua leo jijini Dar es
Salaam.Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Kazi Dunia Tanzania Bw,Jealous
Chirove.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Dk. Abdallah Possi akimkabidhi ripoti
ya matokeo ya utafiti wa utumikishwaji
wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara mwakilishi wa Shirika la kazi Duniani,Geneva
Bw.Azfar Khan leo jijini Dar es Salaam
Serikali imesema kuwa itaendelea kupambana na
kupinga utumikishwaji wa watoto nchini ili tuwe na Taifa imara.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu Dk.Abdallah Possi alipokuwa
akizindua ripoti ya matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014
Tanzania Bara Jijini Dar es Salaam ambayo imeonyesha kuwa utumikishwjai wa
watoto umepungua kutoka asilimia 30.1 mwaka 2006 mpaka asilimia 28.8 mwaka
2014.
Dk Possi alisema kuwa Jitihada mbalimbali zinaendela
kufanywa na serikali ya awamu ya Tano ikiwemo utoaji wa Elimu bure ili
kuhamasisha mahudhurio ya watoto shuleni na kupunguza uwezo wa watoto
kujihusisha na ajira za utotoni.
Aidha Naibu Waziri uyo alisema kuwa utafiti huo
umebaini kuwa takribani watoto milioni 5 wanajihusisha na shughuli za kiuchumi,
miongoni mwao wasichana ni asilimia 52.5
na wavulana ni asilimia 47.5 ambayo kwa ujumla katika watoto wa tatu mmoja
anajihusisha katika shughuli za kiuchumi uku sekta ya kilimo,misitu na uvuvi
ndo zimebeba asilimia 92.1 ya watoto wote wanaojihusisha na shughuli za
kiuchumi.
Aidha ripoti hiyo imeonyesha kuwa watoto
wanaotumikishwa vijijini ni wengi kuliko mijini na hivyo maendeleo ya kiuchumi
ni muhimu katika kuhakikisha ajira kwa watoto zinatokomezwa na kwa hili
serikali inaendelea kuhakikisha kuwa elimu na maendeleo vijijini yanapatikana
ili kuondoa tatizo hilo.
Kwa upande wa elimu ripoti inaonyesha kuwa watoto
wanaoishi mijini hutumia muda mwingi kujisomea tofauti na walioko vijijini
ambapo watoto wanaoishi Dar es Salaam hutumia muda mrefu zaidi katika kujisomea
ambapo ni sawa na asilimia 19.9 ikifuatiwa na maeneo mengine ya mjini ambao hutumia
asilimia 17.8 ya muda wao kwa siku kwa kujisomea na watoto wa vijijini
walitumia asilimia 14.4 kwa ajili ya shughuli za kujisomea.
Naye Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt
Albina Chuwa amesema kuwa ripoti hii itasaidia katika kutengeneza sera nzuri za
maendeleo na kudai kuwa kila mtu ana jukumu la kuhakikisha watoto wanalindwa na
kuacha kutumikishwa katika shughuli za kiuchumi na pia taasisi yake imejiandaa
vyema katika kutumia mfumo mpya na wa kisasa unaoitwa E-popular register ili kupata takwimu ambazo zinaendana na wakati.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Watoto
Duniani(UNICEF) Bi.Cecilia Baldeh amesema kuwa asilimia 29 ya watoto duniani
wanatumikishwa katika shughuli za kiuchumi na hivyo kukosa haki yao ya msingi
ya kusoma na kuiomba serikali kufuatilia kwa karibu mazingira ya kazi
yanayohusisha watoto na kushauri kuwekwa kwa mfumo wa kijamii ambao utasaidia
kufatilia na kuwalinda watoto katika
Nyanja zote.
No comments:
Post a Comment