Mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali mstaafu Ezekiel
Kyunga amewaagiza wakuu wapya wa wilaya
zote mkoani Geita kuhakikisha wanadhibiti
suala la watu ambao wamekuwa wakiingia
mkoani hapa kutoka nchi jirani
kinyume na taratibu za sheria ya nchi
kwa kushirikiana na kamati za ulinzi na usalama zilizopo katika wilaya
wanazoziongoza.
Kyunga
ameyasema hayo jana katika Hafla fupi ya
kuwaapisha wakuu wa wilaya tano zilizopo mkoani hapa iliyofanyika katika ukumbi
wa ofisi za mkuu wa mkoa
Amesema kuwa
suala la ulinzi na usalama ni muhimu sana katika jitihada za kuleta
maendeleo ya wananchi hivyo ni vyema wakawa makini kwa kudhibiti mipaka ya
wilaya zao ikiwa ni pamoja na kuwadhibiti
wageni wanaoingea nchini kwa njia za zisizo halali.
aidha Kyunga ameendelea kuwaagiza wakuu wa wilaya
kuakikisha wanasimamia taratibu mbali mbali za kuhakikisha wanatokomeza ujambazi
ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kushirikiana na
mabalozi wa nyumba kumi ambao wamekuwa wakihakikisha wanalinda maeneo
wanayoyaongoza katika mitaa yao.
Hata hivyo miongoni mwa wakuu wa wilaya hao kutoka
katika wilaya ya Geita na Mbongwe Herman
Kapufi na Matha m Mkapusi wamesema kuwa
ili kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa ni vyema wananchi wawaunge mkono
ili kuhakikisha uhalifu unatokomezwa.
No comments:
Post a Comment