Wednesday, 13 July 2016

NGASSA KUHAMIA MOROKA SWALLOWS, TIMU YAKE YAUZWA AFRIKA KUSINI


MAKUBALIANO yamefikiwa klabu ya Free State Stars ya Bethlehem anayochezea kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa kununuliwa na Moroka Swallows ya Johannesburg, Afrika Kusini .

Ngassa amesema kuwa leo kutoka Afrika Kusini kwamba ni kweli kuna mpango huo na wanatarajia kupewa taarifa rasmi leo.
"Tumeambiwa tutakuwa na kikao leo saa nane, lakini tayari habari zimevuja timu inauzwa, ila tutajua rasmi kwenye kikao,"amesema Ngassa leo baada ya kurejea kutoka kwenye mazoezi ya asubuhi mjini Bethlehem.
Baada ya kushuka daraja kwa mara ya pili ndani ya misimu miwili, mwishoni mwa msimu wa 2015/2016, Swallows imekuwa ikifanya mipango ya kununua nafasi ya kurejea Ligi Kuu na klabu mbalimbali.
Na sasa kwa mujibu wa habari za ndani mpango wa kuiuza Stars kwa Swallows umekubaliwa baina ya pande zote, baada ya majadiliano ya kina.
Sasa kinachosubiriwa no bodi ya Ligi ya PSL kuutathmini mpango mzima wa dili hilo na kutoa baraka zake. Na uamuzi wa PSL utazingatia kanuni kama taratibu zote zote zimefuatwa.
Iwapo mpango huo utakubaliwa na bodi ya Ligi, Stars itakuwa timu ya pili kuuzwa tangu mwishoni mwa msimu uliopita, baada ya Mpumalanga Black Aces kuuzwa kutoka kwa Mario na George Morfou kwenda kwa John Comitis - na sasa inajulikana kama Cape Town City FC chini ya mmiliki mpya.
Stars nayo itahamishia maskani yake Johannesburg na kupewa jina jipya la Moroka Swallows iwapo mpango huo utakamilika.
Ngassa alijiunga na Free State Stars msimu uliopita kama mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake Yanga na wakati anajiandaa kuingia katika msimu wake wa pili kwenye mkataba wa miaka minne, timu hiyo inataka kuuzwa.


No comments:

Post a Comment