Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa
ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa
Tanzania na kuwaasa watanzania kudumisha amani ambayo ilipatikana baada ya
Mashujaa wetu kuipigania na hata kujitoa uhai wao kwa ajili ya Taifa.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mheshimiwa Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiongea
leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya
maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kuwataka watanzania
kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Magufuli katika harakati za kuijenga Tanzania
mpya.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
Mheshimiwa Dkt.Ali Mohamedi Shein akiongea
leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya
maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kusisitiza kuhusu
umuhimu wa watanzania kuenzi amani iliyoasisiwa na wazee wetu na kuacha
kushiriki katika vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.
Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Samweli Malechela
akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya
maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kumshukuru kwa
kusimamia na kutekeleza ahadi zilizowahi kutolewa na hayati Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo kuhamishia serikali Mkoani Dodoma.
Waziri Mkuu Mheshimiwa
Kassim Majaliwa akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla
wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na
kumuahidi Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa atahakikisha anasimamia
utekelezaji wa maagizo ya kuitaka Serikali ihamie mjini Dodoma.
Mnara wa Kumbukumbu ya
Mashujaa baada ya kuwekwa kwa silaha za asili za mashujaa na maua
Baadhi ya wananchi
wakifuatilia shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania
katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini
Dodoma wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa
Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli akiweka silaha za asili kwenye Mnara wa Mashujaa leo
Mkoani Dodoma wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya
Mashujaa Tanzania
No comments:
Post a Comment