Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo
akionyesha jalida maalum wakati wa uzinduzi wa mpango wa Nishati endelevu kwa wote(SE4ALL)
wenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nishati yauhakika kufikia mwaka 2030.Kushoto
kwake ni Mratibu mkazi washirika la
umoja wa Mataifa na mwakilishi washirika la Maendeleo la Kimataifa Bw.Alvaro Rodrigez(UNDP)
na Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa benki ya Maendeleo ya Afrika Bi.Tonia Kandiero.
Waziri wa Nishati na Madini
Prof Sospeter Muhongo amezindua mpango wa Nishati endelevu kwa wote (SE4ALL)
wenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika kufikia mwaka
2030, wakati akiindua mpango huo amesema kuwa uwekezaji wa umeme Vijijini awamu
ya tatu utagharimu zaidi ya Trilioni moja.
Mpango huu umelenga kufanikiwa mwaka 2030, lakini
kwa sisi Tanzania kabla ya mwaka huo tutakuwa na umeme kwa kila mtanzania na
Programu hii italifanya taifa letu lijulikane duniani kwani tuna dhamira ya
kumfanya kila mtu apate umeme”
utasaidia
suala la ajira na kutokomeza umaskini, kwaiyo kama nchi tuko katika ngazi za
juu za huu mradi katika kuufanikisha tukishirikiana na wadau mbalimbali
Aidha amesema kuwa Programu hii ya Umoja wa Mataifa
itasaidia sana katika kuongeza vyanzo vya kuzalisha umeme kwani inafanana sana
na ile ya kwetu ya Taifa ambapo tutazalisha umeme mwingi kutokana na gesi,
makaa ya mawe, umeme wa maporomoko ya maji, umeme wa Jua, joto ardhi na mabaki
ya mimea.
Amesema mashirika mengi yamesaidia katika kufanikisha
upatikanaji wa umeme vijijini ikiwemo benki ya Dunia ambayo imetoa dola milioni
200, Umoja wa Ulaya umetoa euro 180, Nchi za Nordic zimetoa dola milioni 300
pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika nayo imetoa fedha katika kuwekeza kwenye
umeme vijijini pia.
No comments:
Post a Comment