Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akizindua Fursa ya Sanaa inayodhaminiwa na
British Council Tanzania 11 Julai, 2016. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Maendeleo ya Sanaa, Bi. Leah Kihimbi, wa pili kulia ni Mkuu wa Masuala ya
Sanaa Kenya na Afrika Mashariki toka British Council, Bi. Rocca Gutteridge na wa
pili kushoto niKaimu Mkurugenzi British Council Tanzania, Bi. Nesia Mahenge.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akiangalia bango lenye ujumbe kuhusu fursaya sanaa
inayodhaminiwa na British Council Tanzania 11 Julai, 2016. Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Bi. Leah Kihimbi, wa pili kulia ni Mkuu
wa Masuala ya Sanaa Kenya na Afrika Mashariki toka British Council, Bi. Rocca
Gutteridge na wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi British Council
Tanzania, Bi. Nesia Mahenge.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Mhe. Nape Nnauye akiimba huku akipiga gitaa mara baada ya kuzindua Fursa ya
Sanaa inayodhaminiwa na British Council Tanzania 11 Julai, 2016 Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye
akiwaonyesha Wageni waalikwa pamoja na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)
picha aliyochorwa na mmoja wa Wasanii mara baada ya kuzindua Fursa ya
Sanaa inayodhaminiwa na British Council Tanzania 11 Julai, 2016 Jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi British Council Tanzania, Bi. Nesia
Mahenge.
Wasanii nchini
wametakiwa kuchangamkia fursa ya kazi za sanaa ambayo inadhaminiwa na British
Council Tanzania.
Wito huo umetolewa leo
Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.
Nape Nnauye wakati wa Uzinduzi wa Fursa ya Sanaa kwa Tanzania na Afrika
Mashariki ambayo Mdhamini wake ni British Council Tanzania.
Mhe. Nnauye amesema
kuwa, uzinduzi wa fursa hiyo utawasaidia wasanii nchini, Mashirika mbalimbali
yakiwemo Makampuni ya ndani ya Tanzania pamoja na Afrika Mashariki pamoja na
Uingereza.
Amesema kuwa, fursa
hiyo ni kubwa kwa wasanii nchini na kwa Taifa kwa ujumla, hivyo ameipongeza
British Council Tanzania kwa kuja na wazo hilo zuri kwa manufaa ya wasanii
nchini.
‘’Napenda nichukue
nafasi hii kuwapongeza British Council Tanzania kwa kuwashirikisha wasanii na
Makampuni mbalimbali na kuhakikisha kuwa fursa hizi zinamfikia kila msanii
ndani ya Tanzania na kuwawezesha kushirikiana pamoja kwenye Sekta ya Sanaa na
Utamaduni ndani ya Afrika Mashariki na Uingereza kwa ujumla’’, alisema, Mhe.
Nnauye.
Ameongeza kuwa
Serikali kupitia Wizara yake imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali ndani na
nje ya Tanzania katika kuwawezesha wasanii katika kukuza vipaji vyao na
kupata fursa zinazowawezesha kuitangaza nchi yao.
‘’Serikali inatambua changamoto
zinazowakabili wasanii wetu na imejikita katika kuhakikisha kuwa inatoa fursa
zilizopo kwa wasanii wetu’’.
Mhe. Nnauye amesema
kuwa, Serikali itaendelea kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba inazidi
kushirikiana na British Council Tanzania na wadau mbalimbali ili kukuza vipaji
vya wasanii hao.
Kwa upande wake Mkuu
wa Masuala ya Sanaa Kenya na Afrika Mashariki toka British Council, Bi. Rocca
Gutteridge amesema kwamba, fursa inayodhaminiwa na British Council inalenga
kuwawezesha Wasanii wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kuwa karibu kwa
kushirikiana katika vipaji vyao na hivyo wameanzisha na platfomu maalum ambayo
wasanii hao watakuwa wakisaidiana katika kazi zao.
Naye Kaimu Mkurugenzi
British Council Tanzania, Bi. Nesia Mahenge amesema kuwa katika kuanzishwa wa
fursa hiyo, kutakuwa na Miradi kati ya mitatu hadi tano ambayo itachaguliwa
katika mwaka wa 2016/17 ambapo kila mradi utapewa fedha kiasi cha
Euro elfu 20.
Ameongeza kuwa,
British Council inalenga kusaidia zaidi ya wasanii 60 wa Afrika Mashariki
ambapo wataweza kusafiri ndani ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha miezi tisa
ijayo.
No comments:
Post a Comment