Akizungumza
wakati wa maombolezo ya kumbukumbu za Mashujaa sambamba na kuwashwa kwa Mwenge
wa Uhuru katika mnara wa kumbukumbu za Mashujaa, leo usiku katika viwanja wa
Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma, Waziri Mhagama
alisema kuwa kufanyika kwa maombolezo ya Mashujaa mkoani Dodoma ni heshima kwa
wananchi wa Dodoma na watanzania wote kwa ujumla.
“Kufanyika
kwa maombolezo haya inatukumbusha
watanzania kuwa wazalendo na kupigania bila kuchoka, bila kujali makabila yetu
na tujifunze kwa Mashujaa hawa waliopigania uhuru wetu” alisema Waziri Mhagama.
Waziri
Mhagama aliwaomba watanzania kutumia
siku ya kumbukumbu ya Mashujaa ambayo ni Julai 25, kwa namna mbalimbali ikiwemo
kufanya maombi ya sala kwa
Mashujaa wote walifariki katika harakati mbalimbali za kupigania uhuru wa Taifa
la Tanzania.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimwa Jordani Rugimbana aliishukuru Serikali kwa uwamuzi wa kuadhimisha
kumbukumbu za mwaka huu za
Mashujaa mkoani Dodoma, na kusema kuwa kufanyika kwa tukio hilo la kihistoria
linakumbusha uwajibu wa watanzania na Mkoa wa Dodoma utaienzi heshima hiyo.
Aidha,
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mheshimiwa Christina Mndeme aliwasha Mwenge wa
Uhuru katika kilele cha mnara wa mashujaa mnano saa 6 kamili usiku ikiwa ni
sehemu ya maombolezo ya
kumbukumbu ya Mashujaa.
Mnara
wa Mashujaa uliopo mkoani Dodoma ni kati ya vituo 4 vilivyopo nchi nzima
ambavyo vimekuwa na makaburi ya Mashujaa mbalimbali waliopigania uhuru wa nchi
ya Tanzania. Vituo vingine vipo meneo ya Mtwara, Dar es Salaam na Kagera.
Maadhimisho
ya kumbukumbu za Mashujaa kwa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika kesho julai 25,
mkoni Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli atakuwa mgeni rasmi.
Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma Mh. Christina Mndeme akiwasha Mwenge wa uhuru katika mnara
wa mashujaa kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mshujaa, hafla iliyofanyika Saa
Sita Kamili usiku ya tarehe 25 julai 2016 Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Mh. Jordan Rugimbana akiongea na baadhi wa viongozi wa serikali
waliohudhuria tukio hilo la uwashwaji wa Mwenge na kumshukuru Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa kuupa heshima Mkoa wa Dodoma wa kuadhimisha siku ya
mashujaa.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama akiongea na baadhi wa viongozi wa serikali waliohudhuria
tukio hilo la uwashwaji wa Mwenge na kutoa rai kwa watanzania kuwa wazalendo na
nchi yao bila kujali itikadi ya mtu kama walivyofanya wazee wetu waliopigania
uhuru wa nchi.
Wanajeshi
wa Kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuwashwa kwa Mwenge kuelekea Maadhimisho
ya Siku ya Mshujaa yatakayofanyika tarehe 25 julai 2016 Mkoani Dodoma.
Baadhi
ya Viongozi mbalimbali wa Serikali wakishuhudia uwashwaji wa Mwenge.
Mwenge wa uhuru mara
baada ya kuwashwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh. Christina Mndeme, Tarehe
25 julai 2016 Saa Sita Kamili usiku Mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment