Friday, 15 July 2016

SIMBA SC YASHUSHA KIFAA KUTOKA CAMEROON, MOJA KWA MOJA KAMBINI MOROGORO


Hiki ndicho kikosi cha Panthere ya Cameroon cha msimu uliopita, timu anayotokea Ndjack Anong Guy Serges
 SIMBA SC imeshusha mtu anaitwa Ndjack Anong Guy Serges kutoka Cameroon ni jukumu lingine la kocha Joseph Marius Omog kumtazama na kuamua kumsajili au la.
Mchezaji huyo kutoka klabu ya Panthere ya kwao, anacheza nafasi za mshambuliaji wa kati na kiungo wa pembeni.
Na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anafanya idadi ya wachezaji wa kigeni waliofika Simba kwa majaribio kufika watano.
Wengine ni mshambuliaji Frederick Blagnon kutoka Ivory Coast, mabeki wa kati Method Mwanjali kutoka Zimbabse, Janvier Besala Bokungu na kiungo Mussa Ndusha wote kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 



Simba SC imeweka kambi mjini Morogoro kujiandaa na msimu mpya na mbali na wachezaji hao wa kigeni, kuna wapya wengine ambao ni pamoja na watatu waliosajiliwa kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, wote viungo Muzamil Yassin, Mohamed ‘Mo’ Ibrahim na Shizza Kichuya.
Wengine ni Moses Chibandu, Said Mussa, Kelvin Falu, Vincent Costa wote wapya pamoja na wa zamani Nahodha Mussa Hassan Mgosi, Juuko Murshid, Vincent Angban, Awadh Juma, Said Ndemla, Peter Mwalyanzi, Peter Manyika, Dennis Richard, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hijja Ugando, Novatus Lufunga, Mwinyi Kazimoto, Danny Lyanga na Ibrahim Hajib.


No comments:

Post a Comment