Mkazi mmoja mkoani
Singida anayedaiwa kuwa daktari feki anatuhumiwa kusababisha kifo cha mgonjwa,
Israel Shabani (68) baada ya kumfanyia upasuaji wa tezi dume.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema jana kuwa tukio
hilo lilitokea Alhamisi iliyopita saa mbili usiku nyumbani kwa mtuhumiwa baada
ya kumfanyia Shabani upasuaji.
Alisema mtuhumiwa huyo
anadaiwa alikuwa akifanya kazi katika vituo vya afya serikalini, lakini baada
ya kuacha alijiita daktari na kuamua kutoa tiba ikiwamo ya upasuaji nyumbani
kwake kinyume na sheria.
Baada ya kumfanyia
upasuaji huo wa kienyeji, mgonjwa huyo alitokwa damu nyingi na kuwa katika hali
mbaya.Mtuhumiwa alipobaini hali hiyo, alimtelekeza na kukimbilia
kusikojulikana.
Alidai kuwa baada ya polisi kufanya upekuzi kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo, walikamata vifaa vingi vya tiba zikiwamo dawa za kutibu binadamu.
Alidai kuwa baada ya polisi kufanya upekuzi kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo, walikamata vifaa vingi vya tiba zikiwamo dawa za kutibu binadamu.
No comments:
Post a Comment