Na, Joel Maduka, Geita.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage
Amesema lengo la Serikali ni kuhamasisha ujenzi wa Uchumi wa
Viwanda Jumuishi ambao unawahusisha watu wengi kupitia viwanda vidogo na vya
kati,vitakavyotumia malighafi zitakozozalishwa hapa nchini vilivyopo katika
maeneo mbalimbali nchini, ukiwepo mkoa wa Geita ambao umeonekana kufanya
vizuri katika eneo hilo.
Waziri Mwijage ameyasema hayo alipozungumza na wadau wa Viwanda, Biashara
na Uwekezaji wa Mkoa wa Geita wakati wa ziara yake Mkoani humo,
ambapo amesisitiza juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda ulio imara,
shindani na endelevu, utakayozingatia mambo muhimu matatu ambayo ni soko,
malighafi na teknolojia.
Sanjali na Hayo Waziri Mwijage amemtaka mkuu wa mkoa
kuhakikisha anasimamia vyema ujenzi wa ofisi za SIDO pamoja ujenzi
wa majengo ya kufundishia wajasiriamali ambayo yanatarajia kujengwa Wilayani
Chato ili kufikia mwezi wa nne ujenzi huo uwe umekamilika .
Pia ameongezea kuwa ujenzi wa ofisi ambazo zitajengwa kwenye eneo la
magogo litakuwa na eneo la kuwafundishia wajasiriamali mbinu mbali
mbali za kuanzisha viwanda vidogo pamoja na namna ya kusindika bidhaa ambazo
wanatakiwa kuziingiza sokoni.
Akiwasilisha taarifa ya Mkoa ,Mkuu wa Mkao wa Geita Mhandisi Robert
Luhumbi, amesema ili kuandaa mazingira mazuri yatakayowawezesha
wawekezaji kuvutiwa na kuwekeza mkoani humo Mkoa umetenga maeneo 384
yaliyopo katika Halmashauri sita yenye ukubwa wa jumla ya ekari 1,012 kwa ajili
ya viwanda na ramani za mipango miji zimeandaliwa .
Luhumbi ametaja mikakati ya mkoa huo kwenye sekta ya viwanda kuwa ni
Kuanzisha kiwanda cha kuchakata muhogo na kufungasha ambapo maghala
mawili ya kuhifadhi muhogo na sokomoja yamejengwa na
kukamilika kupitia Programu ya Uboreshaji wa miundombinu ya masoko uongezaji
thamani na huduma za kifedha vijijini pia Kuanzisha kiwanda cha kusindika nyama
katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ambapo andiko limeandaliwa na
kuwasilishwa katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa ajili ya
kupata mwekezaji.
Ameongezea kuwa Mkoa unaendelea kufanya mazungumzo na wawekezaji
walioonesha nia ya kuwekeza katika kiwanda cha sukari. Aidha, tarehe 02
Januari, 2018 Mkoa umekutana na uongozi wa Bodi ya Sukari Tanzania kwa lengo la
kuanzisha kiwanda cha sukari katika Wilaya ya Geita.
Ofisi hizo zinazotarajia kujengwa kwenye eneo la Magogo kwenye
halmashauri ya mji wa Geita na Wilaya ya Chato zinatarajia
kuwa na maabara ndogo kwa ajili ya uzalishaji,Chumba cha baridi kwa
ajili ya kuhifadhi bidhaa kama maziwa na kadhalika na kutakua na mabanda ya
watakayotumia wajasiriamli kwa muda.
No comments:
Post a Comment