Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa zana haramu za uvuvi kwenye Kijiji cha Nkome Wilayani Geita . |
Wananchi wa Kata ya Nkome wakiwa kwenye mkutano ambao ulikuwa na lengo la kuelezea hali ya uvuvi haramu ilivyo kwenye kata ya Nkome na namna ambavyo oparesheni imeweza kufanyika kwenye maeneo hayo. |
Kiongozi wa kikosi maalumu kinachoendesha oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu ziwa victoria Gabriel Mageni akielezea namna ambavyo wameweza kuendesha zoezi hilo ndani ya siku kumi na mbili. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisita kwa wale ambao ni watumishi na viongozi kuacha kuendelea na tabia ya kushirikiana na wavuvi haramu . |
Serikali Mkoani Geita Imeteketeza zana haramu zenye thamani ya
shilingi milioni therathini na tatu zikiwemo Nyavu za makila
zilizounganishwa 2,393,makokolo ya sangara 32,timba 142 makokoro ya dagaa
7 na dududu 11.
Hatua hiyo imetokana na oparesheni ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi
haramu ambayo inaendelea kwenye maeneo ya ziwa viktoria ikiwa na lengo la
kuondoa uvuvi huo ndani ya ziwa hilo pamoja na kuondoa mitandao ya
wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia ,biashara ya samaki wachanga na
utoroshaji wa samaki na mazao ya yake,kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.
Zoezi hili la uteketezaji zana hizo limefanyika kwenye Kata ya
Nkome ,ambapo kiongozi wa oparesheni hiyo Gabriel Mageni ,amemweleza mkuu
wa mkoa huo kwamba kuna baadhi ya wafanyakazi wa hifadhi ya Rubondo
wamekuwa wakihusika na uvuvi haramu kwa kuwaruhusu wavuvi kuingia kwenye hifadhi
na wengine kuficha zana zao ndani ya hifadhi na kwamba wamekuwa wakilipwa fedha
wafanyakazi hao maarufu kwa jina la "KIFUNDA"
Kufuatia malalamiko hayo mtandao huu umetafuta kwa njia ya simu afisa
mahusiano wa TANAPA Pascal Shelutete alisema kuwa wao kama watu ambao wanamamlaka
ya hifadhi za taifa na kwamba kwa mujibu wa kanuni na taratibu za sheria
askari wao hawapaswi kushiriki kwenye vitendo vya ujangili na kwamba
taratibu za kiuchunguzi zikifanyika na wakabaini kuna watumishi wanajihusisha
na vitendo hivyo hatua za kisheria na za kinidhamu zitachukuliwa na hawawezi
kuwakingia kifua.
Aidha Mageni aliongeza kuwa katika operesheni hiyo ambayo ina siku
kumi na mbili baadhi ya mambo ambayo wameyabaini ni pamoja na baadhi ya
viongozi wa vijiji na maofisa wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa hifadhi raia
wa kigeni wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi wakiwa hawana kibali na
kusababisha serikali kukosa mapato.
Mkuu wa Mkoa huo,Mhandisi Robert Luhumbi,amewataadhalisha watendaji
ambao wanashirikiana na wavuvi haramu na kwamba endapo kuna mtu hakibainika na
kitendo hicho serikali itahakikisha inamchukulia hatua na kwamba kupitia
oparesheni hiyo hatabakia hata mtu mmoja ambaye anajihusisha na shughuli hizo.
Nyawalwa Wange ni moja kati ya watu ambao wanajishughulisha na kazi
ya uvuvi alisema agizo la Mkuu wa Mkoa ni la kuungwa mkono kutokana na
kwamba uvuvi haramu umeendelea kuharibu kwa kiasi kikubwa samaki ambao wapo
ndani ya ziwa viktoria na kwamba serikali iendelee kuwabaini wale wote ambao
wanaendelea kufanya shughuli za uvuvi kinyume na sheria.
Katika oparesheni hiyo jumla ya fedha ambazo zimekusanywa ni zaidi ya milion, 111 fedha zinazotokana na
faini ,malipo ya mrahaba pamoja na mauzo ya samaki.
No comments:
Post a Comment