Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 81 Januari 2018.
Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua mgodi wa kampuni ya uchimbaji dhahabu na Green Garnet ya Gemini Exploration & Mining Services (GEMS) kabla ya kuzungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua baadhi ya maeneo ya uzalishaji madini ya dhababu kwenye kampuni ya uchimbaji dhahabu na Green Garnet ya Gemini Exploration & Mining Services (GEMS) wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.
Kamishna msaidizi wa madini kanda ya kusini Ndg Mayigi Makorobela ameagizwa
kuanzisha haraka ofisi ya Madini Wilayani Ruangwa ikiwemo kupeleka wataalamu
ili kurahisisha huduma za kitaalamu kwa wachimbaji wadogo ikiwemo elimu ya
usalama kazini.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ametoa agizo
hilo leo tarehe 18 Januari 2018 wakati akizungumza na wachimbaji wadogo
waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya
Megembekenyela wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.
Alisema kuwa Wizara ya Madini imeamua kuanzisha ofisi hiyo kutokana na
maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa
aliyoyatoa hivi karibuni wakati alipokuwa ziarani Mkoani humo ambapo alibaini
kuwa wachimbaji wadogo wanapata kadhia kubwa kutokana na umbali wa ofisi kwani
wanalazimika kutumia zaidi ya kilomita 45 kuzifikia ofisi za madini zilizopo
Wilayani Nachingwea.
Alisema kuwa Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa anawapenda wachimbaji wadogo
nchini ambao hata hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John
Pombe Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu alibainisha kukusudia
kuwanufanisha watanzania kupitia rasilimali zao ikiwemo madini.
"Mhe Rais Magufuli anataka wananchi wote wanaoishi karibu na mgodi
kunufaika na rasilimali zao, nyote mtakuwa mashahidi, tangu nchi iliporuhusu
uchimbaji wa madini hakuna manufaa ya moja kwa moja kwa watanzania badala yake
madini yamekuwa yakinufaisha mataifa mengine ambayo baadaye tunayapigia magoti
kuyaomba msaada" Alikaririwa Mhe Biteko huku akipigiwa makofi na wananchi
waliohudhuria katika mkutano huo
Mhe Biteko alisema kuwa lengo la kuanzisha ofisi ya madini katika
Wilayani hiyo ya Ruangwa ni kuwarahisishia wachimbaji kuwa na jukumu moja la
kuchimba na kuuza rasilimali wanazozipata kwani watakuwa sehemu ya kuchagiza
maendeleo sambamba na kuinufaisha serikali kutokana na ulipaji kodi.
Aliwasihi wachimbaji hao kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya
awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kwani tangu ameingia
madarakani katika kipindi kifupi ameimarisha nidhamu mpya kwa kila mtanzania na
usimamizi madhubuti wa rasilimali za Taifa.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko
ameipongeza kampuni ya uchimbaji dhahabu na Green Garnet ya Gemini Exploration
& Mining Services (GEMS) ambayo ni kampuni ya wazawa kwa kufanya kazi kwa
kufuata vyema sheria na taratibu za uchimbaji.
Alisema kuwa kampuni zingine zinapaswa kujifunza kwa kampuni hiyo ya GEMS
kutokana kulipa kodi mbalimbali kwa uwazi na ushiriki wa shughuli mbalimbali za
kijamii ikiwemo kusaidia sekta ya afya, Maji, sekta ya elimu sambamba na
michezo.
No comments:
Post a Comment