Baadhi ya wachimbaji wa kijiji na kata ya Rwamgasa wakiendelea na kazi ya uchanjuaji wa madini ya dhahabu. |
Moja kati ya wamiliki wa mialo ya uchenjuaji wa madini ya dhahabu akionesha risti ambayo sio ya EFD ambayo wamekuwa wakipatiwa baada ya kununua kifaa cha kuzimia moto. |
Eneo la kuchenjulia dhahabu likiwa limefungwa na jeshi la zima moto na uokoaji. |
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Wilayani Geita,Barnabas Mapande akikagua moja kati ya mtungi wa kuzimia moto wakati alipofika kuzungumza na kusikiliza changamoto za wachimbaji. |
Kifaa cha kuzimia moto kikiwa kwenye eneo la kuchenjulia dhahabu. |
Na,Joel Maduka,Geita.
Chama cha mapinduzi Wilayani Geita kimelaani kitendo cha jeshi la zima
moto na uokoaji kuwatoza gharama kubwa bila ya kuwapa stakabadhi za
serikali baadhi ya wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye kijiji cha
Lwamgasa huku wakifungiwa shughuli za uchenjuaji madini hayo
kutokana na baadhi yao kugoma kununua kifaa cha kuzimia moto.
Akizungumza baada ya kufika kwenye machimbo hayo na kujionea namna
ambavyo wachimbaji hao wamefungiwa shughuli zao Katibu Mwenezi wa CCM Wilayani
Humo Bw Jonatham Masele,amesema CCM imesikitishwa na jeshi la zima moto
kuwatoza Sh Lakini moja na elfu ishirini.
“Kiukweli sisi kama chama
tumesikitishwa sanaa na kitendo cha jeshi la zima moto kuuza kwa bei kubwa bila
ya kutoa risti mitungi hii ya gesi ya kuzimia moto na jambo jingine kuwafungia
watu shughuli zao bila ya kuwapa elimu jambo hili sio nzuri tunaomba wajitahidi
kuwaelimisha kwanza awa watu nasio kujichukulia hatua ya kuwafungia” Alisema
Masele.
Bw Lehamu Lugiko , Mzee Mathew Kajoro na Mwananyanzara Hamis
wameelezea sababu kubwa ambayo imeendelea kuwapa mashaka wachimbaji kuwa ni
kuuziwa mitungi ya kuzimia moto bila ya kupewa Elimu ambayo itawasaidia
kupambana na majanga ya moto huku wakisikitishwa na kitendo cha kufungiwa kwa
shughuli zao.
Mkuu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani Geita Bw Elisa Mgisha
amesema wao sio wasambazaji kwani kuna watu ambao ni mawakala na kwamba suala
la risti za EFD inatokana na wafanyabiashara wenyewe na kuhusu kuuziwa kwa bei
kubwa ni kwamba wao wanapotoa kibari cha mawakala yeye ndiye mwenye jukumu la
kupanga bei ya kuuza mtungi vile ambavyo anaonelea.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita Bw Barnabas Mapande amemtaka mkuu wa
jeshi la zima moto kushughulikia tatizo hilo na kuacha kuendelea kuwakandamiza
wananchi na wafanyabiashara pindi wanapokuwa kwenye shughuli zao za kujitafutia
kipato.
No comments:
Post a Comment