Wanafunzi wa shule ya msingi Kalangalala wakiimba wimbo wenye maudhui ya siku ya sheria .
Na,Joel Maduka,Geita.
Wananchi Mkoani Geita Wameiomba Mahakama kutoa
mafunzo ya kutosha kuhusu mfumo mpya wa TEHAMA unaotarajiwa kuanza kutumika
kwenye kesi mbalimbali.
Mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
unatajwa kuwa utaongeza ufanisi kwenye mahakama kwa maana ya kutoa fursa kwa
mwananchi aliye nje ya nchi kutoa ushahidi kwenye mahakama zilizopo nchini.
“Mfumo
unaweza kuwa ni mzuri lakini tatizo ni elimu ni wananchi wangapi wanaelimu na
mambo ya teknolojia kwanza tukiangalia kuna baadhi yao ni waoga hata kufika
kwenye mahakama leo hii unadhani wataujua mfumo huo mimi naomba mahakama itoe
elimu zaidi na sio kusubilia hadi siku ya Mahakam ndio watoe elimu” Alisema
Kimamba Amiri mkazi wa mjini Geita.
“Kuhusu teknolojia ambayo inazinduliwa na
mahakama itatusaidia kwendana na wakati mimi nafikili sasa nchi yetu inakwenda
na mambo ya teknolojia kitu ninachokiomba kwenye mahakama ni kuondokana na
vitendo vya unyanyasaji kwenye maeneo ya mahakamani” Alisema John Matiba.
Hata hivyo Kaimu Hakimu Mkazi mfawidhi
mahakama ya Mkoa wa Geita, Ushindi Swalo ambaye alisema lengo ni
kuondokana na mfumo wa zamani wa kutumia karatasi nyingi na kwamba utaratibu
huo utasaidia kuonesha kesi nyingi kwa urahisi zaidi hata kwa mtu aliyembali
kuona kesi yake kama inaendelea kwenye tarehe husika au imehairishwa.
Aidha mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herma Kapufi
amewataka wananchi kujitahidi kujua sheria kwa kuwa mambo mengi yanaendeshwa kwa
misingi ya sheria.
No comments:
Post a Comment