Afisa elimu wa shule za msingi katika Halmashauri ya
mji wa Geita Bw Yesse Kanyuma amesema Idara yake imeandikisha wanafunzi 7 713
wa Darasa la kwanza.
Bw Kanyuma alisema malengo ni kuandikisha
wanafunzi 10109 na kwamba anaamini malengo hayo yatafikiwa kutokana na
mwenendo wa uandikishaji.
“Zoezi la uandikishwaji linaendelea kwenye
halmashauri yetu na hadi sasa tuna asilimia sabini na tisa (79%) hata hivyo
bado tunamatarajio ya kuandikisha wanafuzi wengi zaidi kutokana na kwamba
zoezi hili linaendelea hadi mwezi March” Alisema
Kanyuma
Hata hivyo mtandao huu umetembelea baadhi ya shule
za msingi mjini Geita na kuzungumza na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya
Nyankumbu Mwl Swalala David na Mwl Mkuu wa shule ya msingi Mbugani Florence
Leonard ambao wamesema changamoto kubwa inayowakabili ni upungufu wa vyumba vya
madarasa.
“Nina vyumba kumi na moja vinavyotumika lakini
idadi ya wanafunzi ni zaidi ya elfu tatu na kitu ,mwaka jana nilikuwa na watoto
elfu tatu na mia tano themanini na saba lakini vyumba ni hivyo hivyo
aviongezeki kwa hiyo kilio kikubwa ni vyumba vya madarasa imefikia hatua
tumeamua kutumia baadhi ya miradi tuliyonayo ili kujenga vyumba vitatu vya
madarasa ingawa na vyenyewe havitoshi kutokana na wengi uliopo wa wanafunzi” Alisema Mwl Swalala.
Aidha Mwl Swalala ameendelea kusema pamoja na
matatizo ya uhaba wa madarasa hata hivyo bado wanakabiliwa na tatizo la
madarasa kuchakaa na kutengeneza nyufa hali ambayo ni hatarishi kwa wanafunzi
ambao wanasoma kwenye madarasa hayo.
“Kutokana na wingi wa wanafunzi imekuwa ni kazi
ngumu sana kwa mwalimu pindi anapofundisha kumpitia kila mwanafunzi na
kumuelekeza hata hivyo pamoja na changamoto hizo walimu wameendelea kujitahidi
kufundisha” Alisema Mwl Leornad
Hata hivyo kwa upande wake Mwl Risa Nkya alisema
idadi kubwa ya wanafunzi madarasani kumekuwa kukiwanyima amani walimu wengi na
kujikuta wakitimiza wajibu tu wakufundisha kwani hali ya mlundikano wa
wanafunzi ni kubwa sanaa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Nyankumbu
akiwemo Devid Cosmas na Devota John wameelezea kuwa hali ya mlundikano ni
tatizo ambalo linaweza kuchangia kushusha kiwango cha cha Elimu kwani wamekuwa
wakishindwa kusoma vizuri kutokana na wingi wa wanafunzi kwenye madarasa ambayo
wanasomea hivyo wameiomba serikali pamoja na wadau kujitoa kwa dhati kutatua
kero ya uhaba wa madarasa shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment