Ugumu wa maisha katika baadhi ya familia Wilayani Nyang’hwale Mkoani
Geita umetajwa kuwa moja ya sababu za wanafunzi wa kike wa sekondari kurubuniwa
na wanaume kwa kuwapa fedha na hivyo kupata mimba za utotoni.
Takwimu za mimba kwa wanafunzi wa kike kwa shule za sekondari na msingi
wilayani humo katika kipindi cha mwezi January hadi Disemba mwaka jana zilikuwa
mimba 52 na kati ya hizo wanafunzi wa Sekondari ni 37 na wa shule ya msingi ni
15 na kwamba wote walipoteza sifa za kuendelea na masomo.
Mkuu wa Wilaya hiyo Bw Hamim Gweyama amesema miongoni mwa mikakati 10
walionayo kwa mwaka huu kupambana na tatizo la mimba mashuleni.
Hata hivyo katika mimba hizo 52, hakuna kesi hata moja iliyohukumiwa hadi
sasa lakini ziko kwenye hatua tofauti, na kesi 45 ziko polisi na upelelezi bado
unaendelea kufanyika na 7 ziko mahakamani ambapo mkuu wa wilaya hiyo amesema
wana mikakati mingi ya kuwalinda watoto wa kike.
Mimba kwa wanafunzi zimetajwa kuongoza katika shule ya Sekondari ya
Msalala ambapo mtandao huu umezungumza na Mkuu wa shule Bw ,David Mayega
alisema kuanzia mwaka 2016 hadi 2017 katika shule hiyo kumekuwepo na mimba
zaidi ya kumi na kitu na sababu kubwa ni umbali ambao wanafunzi wa kike
wamekuwa wakitembea kwaajili ya kufuata Elimu.
Aisha Said ni mwanafunzi wa shule hiyo alisema kuwa muda mwingine
wamekuwa wakifika nyumbani wanakuta hakuna chakula hali ambayo imekuwa
ikipelekea walio wengi kuingia kwenye vitendo vya ushawishi na kurubuniwa na
tamaa ya vitu vidogo.
Hata hivyo wilaya ya Nyang’wale impokea Sh Milioni 150 kutoka
Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ambapo tayari vifaa vimeanza
kununuliwa na wakandarasi wanatafutwa kwa ajili ya kuanza ujeni huo.
No comments:
Post a Comment