Baadhi ya wakuu wa idara pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wakati alipokuwa akizungumza na kuelezea mikakati iliyopo mkoani humo. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiwashukuru wananchi ambao wamekuwa wakijitoa kuunga juhudi za serikali za kuhakikisha kila eneo linatatuliwa changamoto zake. |
Na,Joel Maduka,Geita
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel wakati
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa kwa seekondari hali
sio nzuri ya wanafunzi ambao wametakiwa kuingia kidato cha kwanza kwani hadi
sasa asilimia 46 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza
hawajaripoti shuleni.
Luhumbi ameongezea kwamba suala la elimu ni haki ya mtoto na
hayupo tayari kuona wazazi wanawaozesha ama kuwaajiri kwenye
shughuli za migodi na biashara ndogondogo watoto ambao wanaumri wa kwenda shule
na wamefaulu mtihani wa darasa la saba.
Ameendelea kusema anafuatilia taarifa ya walimu ambao wameonekana
kuwa ni kikwaza kwa kuchangisha fedha na kwamba endapo wakibaini hatua kali
zitachukuliwa na kwamba amesikia kuna baadhi ya shule walimu wameendelea
kuwatoza fedha wanafunzi kinyume na sheria.
katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana wanafunzi 32,110 walifaulu na
kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu lakini hadi kufikia
tarehe 18 janaury mwaka huu wameripoti wanafunzi 17,202 sawa na asilimia
54 .
Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na idara ya elimu mkoa inaonyesha
wilaya ya Bukombe walichaguliwa wanafunzi 3,985 na hadi sasa wameripoti 1,620
sawa na asilimia 41,Chato walichaguliwa 6,449 walioripoti ni 3,691 sawa na asilimia
57,Geita mji walichaguliwa 4,286 walioripoti ni 2,751,sawa na asilimia 64
huku Mbogwe waliochaguliwa ni 3,029 walioripoti ni 1,924 sawa na asilimia 64.
Halmashauri ya Geita vijijini wanafunzi 11,760 walichaguliwa kujiunga
kidato cha kwanza lakini hadi sasa wameripoti wanafunzi 5,872 ambayo ni sawa na
asilimia 50,wilaya ya Nyanghwale 2,601 walioripoti ni 1,344 sawa na
asilimia 52
No comments:
Post a Comment