Sehemu ya madarasa ya shule ya Msingi Mbugani.
Licha ya jitihada
za kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata Elimu bora lakini bado baadhi ya
wazazi na walezi wanaendelea kuwaficha watoto hao ili wasipate Elimu.
Mwalimu wa Elimu
Maalum katika Shule ya Msingi Mbugani mjini Geita Bi Adella Buhabi
amefafanua kuwa bado kunatatiza kubwa kwa jamii ya kutokujitambua
na kujua thamani ya watoto hao hali inayosababisha baadhi ya wazazi
na walezi kuwaficha.
“Tumeendelea na jitihada kadha wa
kadha ya kuwatafuta watoto hawa na kuwaleta shuleni lakini changamoto kubwa
ambayo tunakutana nayo ni kwa wazazi na walenzi kutokuwa tayari kuwaleta watoto
hawa kupata masomo na wengine wamekuwa wakituuliza kama kuna hosteli au
imekamilika ambayo inajengwa ili waweze kuwaleta hali hii imekuwa
ikiwadumaza sanaa watoto wengi” Alisema Mwl Buhabi.
Pamoja na hayo Mwl Buhabi
ameendelea kusisitiza kuwa wanafunzi wenye ulemavu wakiwezeshwa wanaweza
kufanya vizuri zaidi ya wengine wasio na ulemavu.
Mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu
katika shule hiyo, Neema Mtesingwa alisema amekuwa anakerwa na kitendo cha
baadhi ya watu kwenye jamii kuwanyanyapaa na kuwaona kama hawawezi kupata Elimu
itakayowasaidia maishani mwao.
Utafiti uliofanywa
na wataalam wa kimataifa wanaohudumia walemavu wa aina tofauti nchini ulibaini
kuwa asilimia 98 ya makundi ya watoto wenye ulemavu hawapelekwi shuleni
kwasababu mbalimbali ikiwemo dhana pototu katika jamii.
|
No comments:
Post a Comment