Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi
Mhe.Abdallah Ulega leo ameteketeza zana haramu katika Ziwa Victoria zikiwemo
Nyavu za Makila zilizounganishwa 21710 zenye macho madogo,makokolo ya Sangara
695,Timba 690,makokoro ya dagaa 90 pamoja na Pikipiki tano zilizokuwa zikitumia
katika kusafirisha Samaki haramu.
Akizungumza na wananchi wa Mwembeni
Wilayani Chato Mhe.Ulega amewata kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano
chini ya Rais Magufuli kuwafichuwa haralifu hao ili waweze kuchukuliwa hatua za
kisheria ikiwemo kupigwa faini ama kwenda jela.
”Serikali haitamuonea mtu huruma
awe kiongozi au Raia wa kawaida Sheria itachukuwa mkondo wake nia yetu nikuona
Samaki wanaongezaka ziwa Victoria na watu wavue kwa kufuata sheria ili Taifa
liweze kupata mapato pamoja na ajira kwa wananchi mbalimbali” amesema Mhe.Ulega
Aidha Naibu Waziri huyu amewaonya
Wafanyakazi wa Hifadhi ya Rubondo kuacha tabia ya kupewa rushwana wavivu haramu
kwani wamekuwa wakiwaruhusu kuingia kwenye hifadhi na kuwafichia zana zao
wanapomaliza kuvua na kuwapatia fedha laki mbili hadi tatu.
Hatua hiyo imetokana na oparesheni
ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo inaendelea kwenye maeneo ya ziwa
victoria ikiwa na lengo la kuondoa uvuvi haramu pamoja na mitandao
ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia ,biashara ya samaki wachanga na
utoroshaji wa samaki na mazao ya yake,kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.
Aidha kiongozi wa oparesheni bwana Gabriel Mageni aliongeza kuwa
katika operesheni hiyo ambayo ina siku kumi na tatu baadhi ya mambo
ambayo wameyabaini ni pamoja na baadhi ya viongozi wa vijiji na maofisa
pamoja na Madiwani wanaosimamia maeneo ya uvuvi kuwapa hifadhi raia wa
kigeni wanaofanya shughuli za uvuvi wakiwa hawana kibali na kusababisha
hasara Serikali ikiwemo kukosa mapato
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya
Chato ,Shaban Ntalambe ,amewataadhalisha
watendaji ambao wanashirikiana na wavuvi haramu kuwa endapo kuna mtu
hakibainika na kitendo hicho serikali itahakikisha inamchukulia hatua kupitia
oparesheni hiyo hatabakia hata mtu mmoja ambaye anajihusisha na shughuli hizo
awe kiongozi Mkubwa ama mtu wa kawaida.
No comments:
Post a Comment