Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akimuomba Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi ,Isack Kamwelwe kutatua changamoto ambayo imeendelea kuwepo kwenye baadhi ya maeneo katika Mkoa huo. |
Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi ,Isack Kamwelwe akikagua baadhi ya miradi ya maji kwenye kijiji cha imalabupina wilayani chato. |
Na,Joel Maduka,
Waziri wa maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amewataka wakandarasi wa
miradi mbalimbali ya maji kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ili
kuwaondolea wananchi changamoto ya ukosekanaji maji ambayo imeendelea
kuwakabili kwa muda mrefu .
Mhandisi Kamwelwe ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya siku
moja wilayani Chato Mkoani Geita iliyokuwa na lengo la kukagua miradi ya
maji inayotekelezwa wilayani humo.
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Katoro na Buseresere amesema matatizo
ya maji katika miji ya Muganza, Buzirayombo na Buseresere yataanza kufanyiwa
kazi na pindi tu usanifu wa mradi huu utakapokuwa tayari miradi hiyo itaanza
kutekelezwa ili kumaliza kero kubwa ya maji.
Isack Saimon ambaye ni mkazi wa Buseresere amemuomba waziri kuharakisha
zaidi mradi huo ambao ametoa ahadi kwa wananchi hao kwani kwasasa wameendelea
kupata shida kubwa ya kupata maji na kwamba wamekuwa wakinunua ndoo ya maji kwa
shilingi elfu moja hali ambayo inasababisha wasio na uwezo kushindwa.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Gabriel Luhumbi amewasisitiza
wakandarasi wote wa miradi ya maji kutumia vibarua kwa wananchi wa maeneo
husika ambapo miradi hiyo inatekelezwa.
Katika Wilaya ya Chato jumla ya wananchi ambao wamekuwa wakuipata
maji safi na salama ni ni asilimia 41.
No comments:
Post a Comment