Katibu wa chama cha mapinduzi CCM kata ya Buhalahala mjini Geita Lazaro
Kagoma anatuhumiwa kutafuna kiasi cha zaidi ya milioni 20 ambazo
zilitolewa na halmashauri ya mji wa Geita kwa kikundi cha wajasiliamali
Geita (KIWAGE)walipatiwa na halmashauri ya mji wa Geita.
Kagoma ambaye ni Katibu wa Kikundi hicho cha KIWAGE anadaiwa kuwazunguka
wanachama wenzake na kutafuna fedha walizopatiwa kwa ajili ya
manufaa ya kufanya shughuli za ujasiliamali inadaiwa badala yake alizifanyia
matumizi yake binafsi kinyume na matarajio ya kikundi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Shilabela Bw,Elias
Mtoni alisema kikundi hicho kimeonekana kuwa na ujanja
mwingi kutokana na udanganyifu ambao wameweza kuufanya wa kuidanganya
halmashauri ya mji wa Geita na mwisho wa siku kupatiwa fedha kiasi
cha Milioni 45.
Shida Mpondi ambaye ni mkazi wa Geita,ameitaka serikali kufanya uhakiki
kabla ya kutoa mikopo kwenye vikundi kwa maana ya kujildhihirisha na kujua
shughuli ambazo vikundi vinafanya kazi za ujasiriamali ili kuepukana na utapeli
wa namna kama hiyo iliyojitokeza.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Geita Leonard Bugomola amekiri
kupokea malalamiko dhidi ya kikundi hicho huku akisema kwamba Katibu wa Kiwage
amekuwa akiwatishia wanakikundi wenzake wanapohoji fedha walizokopeshwa.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti amejibu tuhuma za kuhusihwa na
kikundi hicho kuwa ni mmoja wa watu aliyekipigia chepuo ili kurudisha fadhila
katika uchaguzi Mkuu mwaka 2015 jambo ambalo amesema sio sahihi kwani fedha
hizo wamekuwa wakikopesha kwa vijana na vikundi ambavyo vimekidhi vigezo pasipo
kubagua itikadi ya vyama vya siasa.
Hata hivyo mtandao huu umewatafuta wahusika akiwemo mwenyekiti na
Katibu wa kikundi hicho kwa njia ya simu na simu zilikuwa zikiita bila
majibu huku ofisi za kiwage zikiwa zimefungwa kwa takribani miezi mitano
sasa.
No comments:
Post a Comment