Mjumbe wa halmashauri kuu ya
Taifa(NEC) Iddi Kassim Iddi akizungumza na wajumbe wa kikao cha
halmashauri kuu ya mkoa ya chama hicho kwenye ukumbi wa halmashauri ya mji wa
Geita.
Kamanda
wa Jeshi la Zima Moto na uokoaji mkoani Geita Bw Elisa Mugisha akizungumza na
waandishi wa habari hivi karibuni wakati alipokuwa akitoa taarifa ya shughuli
ambazo wamezifanya kwa mwaka ambao umemalizika.
Hayo yamesemwa na Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa(NEC)
Iddi Kassim Iddi,wakati alipokuwa kwenye kikao cha halmashauri kuu
ya mkoa ya chama hicho,alisema wao kama chama wamepokea kwa masikitiko makubwa
tuhuma hizo ambazo zimeelekezwa kwenye chama hicho na lengo lilikuwa sio
kuingilia majukumu ya jeshi hilo ila ni kuwatetea wananchi wa Rwamgasa ambao
walikuwa wakiuziwa mitungi kwa bei kubwa bila ya kupatiwa risti ya
serikali.
“Watambue ya kuwa sisi chama na serikali ni kama baba na mwana ni
kwamba ni lazima kuhakikisha kwamba tunafanya kazi kwa pamoja na napenda
kukanisha kuwa sisi hatuna uadui wala na jeshi la zima moto na tunampa siku
saba akiombe radhi chama na viongozi wake kwani namna ambavyo amefanya ni
kuchafuana”Alisema Kassim.
Aidha Katibu mwenezi wa chama hicho Mkoani humo,Devid Azaria
,amekanusha juu ya tuhuma za viongozi wa chama kuingilia zoezi lao
na kwamba wanachokikataza ni taratibu ambazo zilitumika za uuzwaji wa
vifaa vya kuzimia moto kuwa zilikuwa za kuwalazimisha wachimbaji bila ya kuwapa
elimu jambo ambalo sio sahihi.
Hata hivyo mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Humo.Alhaji Saidi Karidushi
amewataka viongozi wote kufanya kazi kwa kutimiza majukumu yao na kwamba kama
kuna tatizo ni vyema wakayashughulikia wao bila ya kutegemea nguvu kutoka
kwake.
Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Zima Moto na uokoaji mkoani Geita Bw
Elisa Mugisha alipopigiwa simu na mtandao huu amekiomba radhi chama cha
Mapinduzi huku akisisitiza kuwa baadhi ya viongozi wanaomiliki makarasha
kulipia tozo zinazotakiwa na jeshi la zima moto ili kuepusha mtafaruku baina ya
pande hizo mbili.
No comments:
Post a Comment