Baadhi ya viongozi wa chama Tawala pamoja na Diwani wa Kata ya Buseresere Godfey Miti wakishiriki kwenye shughuli ya ufayatuaji matofari. |
Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye shughuli ya uchimbaji wa mchanga wa kujengea madarasa ya shule ya sekondari ambayo ni mpya. |
Diwani wa Kata ya Buseresere,Godfrey Miti akielezea namna ambavyo wananchi wameguswa kushiriki ujenzi wa shule kijiji cha Mulanda. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akikusanya michango kutoka kwa wadau mbali mbali wa maendeleo ambao walikuwa wamejitolea kuchangia ujenzi wa shule hiyo. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Robert Luhumbi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wakiwemo na viongozi .
Na,Joel Maduka,
|
Ikiwa leo Tanzania imeadhimisha miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar ,serikali Mkoani Geita imetumia siku hiyo kwa kushirikiana na wananchi wa Mulanda Kata ya Buseresere kufanya shughuli za maendeleo za ujenzi wa shule ya sekondari kijijini hapo.
Ujenzi huo ambao umeasisiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert
Luhumbi kwa kushirikiana na wanakijiji wa kijiji hicho umetokana na adha
ambazo wamekuwa wakizipata wanafunzi ambao wanasoma shule ya sekondari ya
Buseresere ambao wamekuwa wakitembea umbali wa kilomita sita kufuata elimu.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata ya
Buseresere,Godfrey Miti ,alisema maamuzi hayo ambayo yalichukuliwa na wananchi
yametokana na kwamba kata hiyo inawananchi wengi na kwamba shule iliyopo
ilikuwa haitosho kutokana na kwamba wanafunzi wa kidato cha kwanza 736
ambao wanatarajia kusoma kwenye shule ya kata hali ambayo inaonesha kuwepo kwa
wanafunzi wengi zaidi na kwamba kukamilika kwa shule hiyo itasaidia kupunguza
wingi wa wanafunzi kwenye shule ya sekondari Buseresere.
Aidha kwa upande wake mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ,ambaye
ni mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi,aliwataka wananchi kutambua
kuwa akuna mgeni ambaye anaweza kuleta maendeleo na kwamba maendeleo yanaitaji
kuwa na mapinduzi ya kifikila huku akiwashukuru wananchi kujitoa kwenye ujenzi
wa shule hiyo.
Mhandisi,Luhumbi ameongezea kuwa matarajio ni kuona ifikapo
mwishoni mwa mwaka 2018 kila kijiji kinakuwa na zahahati ili kuhepukana na
usumbufu wa wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Maadhimisho ya miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar, mapinduzi
yaliyoshuhudia kuangushwa kwa utawala wa Sultan na familia yake January 12
mwaka 1964.
Mwaka huu yamefanyika huku Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ikiwa
imepiga hatua katika kupambana na umasikini na kuimarisha demokrasia licha ya
changamoto kadhaa za kisiasa zinazoendelea kushuhudiwa.
Wazanzibari wanaona siku hii inapaswa kutumiwa na Serikali kujitathmini
kuangalia hatua walizopiga na changamoto ambazo zinaendelea kuikabili Zanzibar.
Zaidi ya wanamapinduzi 800 walishiriki kwenye mapinduzi hayo yaliyoifanya
Zanzibar kuwa huru kutoka kwa utawala wa Kisultani.
Sherehe za leo zimejumuisha vikosi vya ulinzi na usalama sambamba na
maandamano ya wananchi wa mikoa mitano ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment