Tuesday, 23 January 2018

BILIONI 3 ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI MKOANI GEITA ZINATARAJIWA KUBORESHA MIUNDOMBINU KATIKA VITUO SABA VYA AFYA

DSC_0527
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki kuchimba msingi kwenye kituo cha afya cha Masumbwe Wilayani Mbongwe.

DSC_0529
Wananchi wakishiriki kwenye ujenzi wa msingi kwenye kituo cha afya cha Masumbwe Wilayani Mbongwe.

DSC_0540
Mkuu wa Wilaya ya Mbongwe ,Mathar Mkupasi akizungumza na wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kuunga mkono jitihada za serikali za ujenzi wa jengo la kupasulia kwenye kituo cha afya cha Masumbwe.

DSC_0557
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM,Wilayani Mbongwe Johari Juma akisisitiza wanachama wa chama hicho kuwa mstari wa mbele kushiriki katika shughuli za maendeleo.

DSC_0570
Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza namna serikali ilivyojipanga kupunguza changamoto ya huduma za afya Mkoani humo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mbongwe.

DSC_0625


Na,Joel Maduka,Geita.



Jumla ya Sh Bilioni 3 zilizotolewa na serikali Mkoani Geita zinatarajiwa kuboresha miundombinu katika Vituo saba vya afya .

Mganga mkuu wa Mkoa wa Geita Dr Japhet Simeo alisema   lengo kuu la hizo fedha ni kuboresha  miundo mbinu kwa maana ya chumba cha upasuaji kujenga wodi ya watoto,wakina mama ,maabara na chumba cha kuhifadhia maiti na kwamba wanatarajia kuona fedha hizo zinafanyika kuboresha mandhari ya kituo kwa maana ya bustani na majengo ambayo yamechakaa.

Simeo alizitaja wilaya ambazo zimepatiwa fedha hizo ni wilaya  5 ikiwemo halmashauri ya wilaya ya  Geita ambayo imepewa kiasi cha sh ,Milioni 500 kwenye  kituo cha afya cha Nzera na kwamba hadi sasa wameshajenga  majengo manne ambayo yamekaribia kukamilika , Mbogwe milioni 800 ambazo zimegawa kwenye vituo viwili vya afya, Bukombe  milioni 400 kwaajili ya kituo cha afya cha uyovu , Chato  wamepatiwa fedha kwaajili ya vituo viwili ambvyo ni Bwanga Milioni 500 na Karumwa milioni 400 na Wilaya ya Nyang’hale milioni 400 kwaajili ya kituo cha afya cha Nyang’hale.

Juma Mabura ni moja kati ya wananchi wa Wilaya ya Mbongwe ambapo ameelezea kuwa kumekuwape na changamoto kubwa ya upungufu wa majengo na kwamba kukamilika kwa baadhi ya majengo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma ya afya.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi amesema kuwa majengo yaliyo kwenye hatua ya renta na maboma yakikamilika watakuwa kwenye asilimia 55 kwa maana ya zahanati 262 na kwamba nyingine wameanza ujenzi .


Aidha amesisitiza kuwa lengo la serikali ni kuondoa kero ya kimiundombinu kwenye sekta ya afya ili kuwawezesha watanzania kupata huduma bora za afya.

No comments:

Post a Comment