Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constatine Kanyasu
akizungumza na wananchi wa mtaa wa Nyamalembo kata ya Mtakuja wakati wa mkutano
wa kiutendaji ambao ulikuwa na lengo la kusikiliza kero zao.
Wananchi wa mtaa wa Nyamalembo wakimsikiliza mbunge
wakati alipokuwa akizunguza nao juu ya suala la maendeleo pamoja na changamoto
ambazo wanazipata kutokana na mgodi wa GGM.
Wakizungumza kwenye mkutano wa maendeleo katika mtaa huo mbele ya mbunge
wananchi hao Bw Charles Methew na Juma Bakari wamesema wameendelea kupokea
ahadi za viongozi uong kutoka kwa viongozi ambao wamekwisha kuja kwenye
maeneo yao na kujionea namna ambavyo mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM)ulivyo
haribu makazi yao kutokana na shughuli ambazo wanazifanya za ulipuaji wa
miamba pia wameelezwa kusikitishwa na namna ambavyo wamekuwa wakizuiliwa kulima
kwenye maeneo hayo na pindi wanapokamatwa wamekuwa wakipigwa na askari wa mgodi
hali ambayo wamemwambia mbunge kua imekuwa ikiwaumiza sanaa.
Diwani wa Kata ya Mtakuja Bw Constatine Molandi alisema mwambia Mbunge
kuwa licha ya neema ya uwepo wa mgodi wananchi ambao wanauzunguka mgodi huo
wanamatatizo makubwa sanaa na kwamba kilio chao kilishawai kufikishwa kwa Rais
Magufuli lakini bado wameendelea kuonewa na kunyimwa fidia na watu wa mgodi huo
ali ambayo imesababisha kujiona kama vile wao sio watanzania.
Kufuatia malalamiko hayo Mbunge wa Geita Mjini Bw Constatine Kanyasu
amewataka wananchi wa maeneo yaliyoathirika kutokana na shughuli za mgodi
wa dhahabu wa GGM kuwa wavumilivu kwani madai yao ya kulipwa fidia yamefikishwa
kwenye wizara husika na kwamba madai hayo yatafika na kwa mheshimiwa Rais John
Magufuli.
No comments:
Post a Comment