Waziri wa maji na umwagiliaji Bw Isack Kamwelwe akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi wakati alipowasili kwenye ofisi za Mkoa huo. |
Waziri wa maji na umwagiliaji Bw Isack Kamwelwe ,akisalimiana na mbunge wa Jimbo la Busanda Lolesia Bukwimba wakati alipowasili kwenye ofisi za Mkoa wa Geita. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi akielezea hali ilivyo ya upatikanaji wa maji wakati wa kikao na wadau wa sekta ya maji Mkoani humo. |
Waziri wa maji na umwagiliaji Bw Isack Kamwelwe,akizungumza na wadau wa sekta ya maji kwenye ukumbi wa mikutano wa mkoa wa Geita. |
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM)Mkoa wa Geita,alhaji Said Karidushi akiwasisitiza watumishi kusimamia kwa makini zaidi miradi ya maji iliyopo kwenye Mkoa huo. |
Waziri wa maji na umwagiliaji Bw Isack Kamwelwe akiwa kwenye mradi wa maji uliopo kwenye kata ya Kalangalala. |
Waziri wa maji na umwagiliaji Bw Isack Kamwelwe ameeleza kusikitishwa
na kitendo cha kutokamilika kwa miradi ya maji ya Inchukimya
Bulamabupina, Nchankolongo na Nyamtukuza licha ya serikali kutenga fedha nyingi
kugharamia miradi hiyo.
Akizungumza na wadau wa maji, Mkoani Geita katika ukumbi wa Ofisi ya Mkoa
huo Bw Kamwelwe amesema amesikitishwa na mradi wa wilaya ya Nyang'hwale ambao
umegaramiwa Sh Bilioni 15 ambao hadi sasa umeshindwa kukamilika licha ya
mikataba zaidi ya kumi na moja kusainiwa.
Amesema lengo la serikali ni kuona kufikia mwaka 2020, Watanzania
hususani wa vijijini wamepata Asilimia 85 ya maji safi na salama.
“Mimi nimepewa dhamana ya kuhakikisha
watanzania wanapata maji safi na salama na ifikapo mwaka 2020 vijijini wapate
asilimia themanini na tano kwasababu serikali yetu inatenga bajeti ya
utekelezaji wa miradi hii” alisema Kamwelwe.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi amemwambia Waziri kuwa
mkoa huo una tatizo la upatikanaji wa maji kwenye maeneo mengi licha ya
kuzungukwa na chanzo kikubwa cha maji ya ziwa viktoria.
Mbunge wa Busanda Lolesia Bukwimba akizungumza kwa niaba ya wabunge wa
Mkoa huo, alisema anaamini ziara ya Waziri wa maji na umwagiliaji itasaidia
kutatua kero ya maji inayowasumbua wananchi kwa muda mrefu kwenye mkoa huo .
Waziri wa maji na umwagiliaji Bw Isack Kamwelwe yuko Mkoani Geita kwa
ziara ya siku 4 yenge lengo la kukagua miradi ya maji
No comments:
Post a Comment