Shirikia lisilo la kiserikali la JSI limetoa Baiskeli 32 na makabati 13
kwa ajili ya kuendeleza mapambano dhidi ya unyanyasaji wa watoto wanaoishi
kwenye mazingira hatarishi .
Akizungumza baada ya kugawa Baiskeli hizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Geita, Mkurugenzi wa JSI kanda ya ziwa Dr Amos Haki Nsheha amesema
wilaya hiyo ina watoto wengi wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Alisema watoto hao wanafikia karibu elfu 20 na kwamba kutokana na
mazingira wanayoishi wana hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi
kutokana na kufanyiwa vitendo viovu ikiwemo kubakwa.
Afisa ustawi wa Jamii wa wilaya ya Geita Bw Anderson Shimbi amesema
matukio ya ukatili kwa mwaka jana yalikuwa 97 kutoka kata 37 ambapo wanaume ni
40 na wanawake 57 na kwamba ukatili unaofanywa zaidi ni vipigo, ubakaji na wengine
kutopewa nafasi ya kwenda shule .
Mmoja kati ya wasimamizi wanaotoa huduma kwa watoto wanaoishi kwenye
mazingira hatarishi, Bw Tom Jarusinga amesema msaada huo umetolewa katika
wakati muafaka kwani wengi wao walikuwa na shida ya usafiri wa kuwafikia watoto
wanaofanyiwa ukatili.
Mkurugenzi wa Halmashauri wa wilaya ya Geita Bw Ali Kidwaka amesema
mchango huo utasaidia kuelekea kwenye malengo ya dunia ya kupambana na ukimwi
na kufikia malengo ya asilimia 90 ya watu wote wenye maambukizi kujua hali zao.
No comments:
Post a Comment