Moja kati ya madarasa ya shule ambayo mkuu wake analalamikiwa na wananchi kuwatoza michango mbali mbali. |
Tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani chini ya Rais Dr John
Pombe Magufuli kupitia wizara ya elimu, sayansi na ufundi ilitoa waraka wa
elimu bure kuanzia elimu ya msingi mpaka kidato nne.
Akizungumzana Storm HABARI , Bi
Odest Timoth alisema kuwa wamekuwa wakitozwa fedha pindi wanapopeleka watoto
wao kuwaandikisha na wanapogoma kutoa wamekuwa wakirudishwa na Mkuu wa
shule na huku wanatambua kuwa serikali imetoa kibali cha wanafunzi kusoma
bure bila ya kutoa pesa hivyo hali hiyo imeendelea kuwachanganya.
“Hali hii sio nzuri kabisa serikali imesema watoto wasome bure leo
hii wazazi tunalazimishwa kutoa michango tena pindi tu unapopeleka mtoto mimi
naomba mkuu wa wilaya hatusaidie juu ya huyu mwalimu maana imeshakuwa ni
kero”alisema Bw Peter John .
Diwani wa Kata ya Buhalahala Bw Mussa Kabese alisema amekuwa
akipokea simu za wazazi wakimlalamikia Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi 14
Kambarage kuwaomba wazazi kiasi cha shilingi elfu kumi na pindi wanaposhindwa
kutoa amekuwa akiwafukuza watoto shuleni hapo jambo ambalo sio sahihi.
Kufuatia tuhuma hizo mtandao huu umemtafutta Mwalimu Mkuu Jacob Bossco
ambaye ni mwalimu mteule wa kusimamia shule hiyo akitokea shule ya msingi
Mbugani ambapo , amekanusha kuhusika na tuhuma hizo na kuelekeza tuhuma
hizo kwa kamati ya ujenzi pamoja na ofisi ya Serkali Mtaa wa 14 Kambarage.
Kutokana na madai hayo Mkuu wa Wilaya Mwl. herman kapufi . amepiga
marufu kwa Walimu Wakuu wa shule za Sekondari na Msingi wilayani humo
ambao wanajihusisha na upokeaji wafedha kutoka kwa wanafunzi kama michango na kwamba
watakao bainika watachukuliwa hatua.
Shule hiyo mpya ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na
fedha kutoka serikalini bado haijafunguliwa kutokana na baadhi ya
miundombinu vikiwemo vyoo kutokamlika licha ya kuandikisha wanafunzi wa darasa
la kwanza.
No comments:
Post a Comment