Friday 29 September 2017

BENKI YA NMB YAZUNGUMZA NA WALIMU MKOANI GEITA



 Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB Omar Mtiga  Akizungumza na walimu wakati wa Kongamano ambalo limeandaliwa na NMB Kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Geita. 




 Baadhi ya walimu ambao wanatoka kwenye halmashauri zilizopo Mkoani Geita wakifuatilia Hotuba ya Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB Omar Mtiga. 



 Meneja wa Benki  ya NMB  Mkoani Geita Mathias Nkuliwa akizungumza wenye Kongamano hilo ambapo alisema lengo la kungamano hilo ni kutambua mchango wa walimu katika Benki ya NMB. 



 Meneja  wa NMB Kanda ya ziwa Abraham Augustino  akizungumza na walimu wakati wa 
Kongamano. 





 Meza Kuu ikiongozwa na Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Geita  wakimsikiliza meneja wa kanda wakati alipokuwa akizungumza. 





 Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB Omar Mtiga  Akizungumza na walimu wakati wa Kongamano ambalo limeandaliwa na NMB Kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Geita. 






 Baadhi ya wafanyakazi wa NMB wakisikiliza maelezo ya  Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB Omar Mtiga  wakati akizungumza kwenye Kongamano hilo.




 Mkuu wa Mkoa wa Geita  Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ambaye alikuwa Mgeni Rasmi akifungua Kongamano la walimu na Benki ya NMB  ambalo limefanyika kwa mala ya kwanza Mkoani Geita. 





 Baadhi ya wadau wa idara ya Elimu Mkoani Geita wakimtegea sikio Mgeni Rasmi. wakati alipokuwa akizungumza na walimu pamoja na wafanyakazi wa NMB Mkoani Geita. 



 Mkuu wa Mkoa  wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa NMB. 






 Mkuu wa Mkoa  wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa Elimu wa Wilaya mbali mbali zilizopo Mkoani Geita.





 Mkuu wa Mkoa wa Geita akiondoka na kuagana na Wafanyakazi wa NMB baada ya kuwa amefungua Kongamano hilo.  


Imebainika kuwa bado kuna idadi kubwa ya watanzania wasiotumia mifumo rasmi ya kifedha na kibenki , ambapo tafiti zinaonesha zaidi ya asilimia ishirini (20)  ndio  wanaotumia huduma za kibenk  huku  sababu kubwa ya kutokutumia ni ukosefu wa elimu na ufahamu wa kutosha kuhusu huduma za Kibenk.

Akizungumza  na Walimu ambao walikuwa kwenye kongamano la siku ya walimu Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amesema kuwa ipo sababu ya kuvishawishi vyombo vya kifedha na taasisi nyingine husika kuwa na program maalumu za kutoa Elimu ya masuala ya kifedha hususani maeneo ya vijijini.

“Hivyo basi kuna kila sababu ya kuvishauri vyombo vya fedha na taasisi nyingine husika kuwa na program maalumu za kutoa elimu ya masuala ya kifedha hususani maeneo ya vijijini ili watanzania walio wengi zaidi waweze kunufaika na maendeleo yaliyofikiwa na sekta ya fedha hapa nchini”Alisema Kyunga.

Aidha kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB Omar Mtiga amesema kuwa idadi ya watanzania karibia milioni 50  ni asilimia 20 tu ndio wenye akaunti za benki , na zaidi ya asilimia 60 ya wananchi wanamiliki simu za mkononi na wana uwezo wa kufanya malipo na miamala kupitia simu za mkononi.

“NMB kwa sasa inaamini katika kutoa huduma za kibenki za kidigitali kwa watanzania wote ,njia hii tunaiona ni bora zaidi na inaendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia na itasaidia kuleta mwamko mkubwa zaidi kwa watanzania wengi kuweza kutumia huduma za kibenki kwa kufanya miamala na malipo mbali mbali”Alisema Mtinga .

Mtinga ameendelea kuelezea kuwa  wateja walionao ni zaidi ya milioni 2.5 kati yao zaidi ya wateja milioni 2 wanatumia simu za mkononi kufanya miamala na kuangalia salio ,kufanya malipo mbalimbali kama kulipia umeme hata kulipia kodi mbalimbali.


Aidha kwa upande wake Mwalimu Imani Amisi ameelezea kuwepo kwa changamoto kubwa ya kimikopo hususani katika taasisi za Kifedha  kuwepo kwa riba kubwa hali ambayo inasababisha wengi wao kushindwa kukopa fedha hizo lakini kutokana na maelekezo ambayo wamepatiwa na NMB wanaamini kuwa Benki hiyo itakuwa mkombozi katika maswala ya Mikopo.


No comments:

Post a Comment