Monday 26 February 2018

WANANCHI WAMLILIA NAIBU WAZIRI NYONGO WALALAMIKA KUCHELEWESHEWA FIDIA

Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo  akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ziwani  kata ya Nyarugusu Wilayani Geita ambao walipatwa na majanga ya kutilikiwa kwa maji yenye sumu kutoka kwenye Bwawa la mgodi wa Nyarugusu mine.

Msemaji Mkuu wa wahanga hao akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo ambapo alielezea namna ambavyo kwasasa wameendelea kuishi maisha ya shida hali ambayo imepelekea wakaandamana na kufunga barabara na kuhamua kulala hapo kwa takribani siku tano wakidai walipwe fidia zao.

Mzee Slvanus Matanywa akilia mbele ya  Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo kutokana na kucheleweshewa fidia zao kwa muda mrefu.

Wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo wakati alipokuwa akitia maelekezo.

Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo,akizungumza na moja kati ya wakina mama ambao wanamadai ya kulipwa Fidia.

 Wananchi wakifungua njia ya barabara ya kutoka mgodini baada ya kuagizwa na Naibu waziri Staslaus Nyongo.

Katibu wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Geita,Julius Peter (Kulia )akizungumza na Naibu waziri wa madini wakati alipofika na kuzungumza na wananchi.

Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo,akikagua na kuangalia Bwawa ambalo limesababisha athari kwenye mazao ya wananchi.

Naibu waziri wa madini Staslaus Nyongo Akizungumza na mmoja wa wamiliki wa mgodi huo Bw ,Alex Kindersley.
Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo amewataka wamiliki wa mgodi wa Nyarugusu Mine  Company kuwalipa  fidia haraka  iwezekanavyo  wananchi 133 ambao wapo kwenye kijiji cha Ziwani kata ya Nyarugusu Wilayani Geita kutokana na kuharibiwa mazao yao na sumu ambayo ilitoka kwenye  Bwawa la maji yenye sumu.
Agizo hilo ambalo amelitoa Naibu waziri wa madini Nyongo limetokana na Wananchi hao ambao wanadai kulipwa fidia ya kiasi cha sh,milioni 202 kufunga barabara ya mgodi huo tangu Februari 18,mwaka huu kufuatia Mgodi huo kutoa majibu yenye utata.

Bi, Pili Ramadhani alisema walipatwa na majanga hayo   novemba 30 mwaka jana baada ya mazao yao kuharibiwa,na kwamba  wamekuwa wanakabiliwa na njaa,hali ambayo imesababisha kuhamua kuandamana huku wakikaa takribani wiki nzima kwenye maeneo ya nje ya mgodi huo wakiitaji walipwe madai yao.

Mzee Slvanus Matanywa (88)  mkazi wa kijiji cha ziwani amejikuta akiangua kilio mbele ya Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akililia fidia yake kutokana na kukabiliwa na njaa kwa kukosa chakula baada ya mazao yake kuharibiwa na sumu hiyo.

 “Nalia kwasababu wajukuu wangu awasomi kutokana na kulala na njaa kwanini imekuwa namna hiyo sasa  sijui nifanyeje sina chochote cha kunisaidia watoto wakianza kulia nashindwa nifanye nini wewe ndiyo Baba maana tumeambiwa tuheshimu mamlaka iliyo juu” Alisema Mzee Matanywa.

Nae Mwenyekiti Wa Kijiji  hicho Athuman Seleman alisema  ni kweli wananchi wake tangu  November mwaka jana mashamba yao yaliingiliwa na matope yenye sumu na serikali  imeendelea na jitihada  za awali za kufanya mazungumzo na  mgodi  ili walipe fidia   shida ilikuja baada ya wamiliki wa mgodi kuleta barua ya kusema hawawezi kutoa fidia kwa sasa mpaka wajiridhishe kutokana na vipengele fulani hapo ndio lililipokuja tatizo.


 “Shida iliyokuja ni kutokana na mgodi kugoma kutoa fidia kwa madai wanataka baadhi ya vipengere wajiridhishe suala hili limewakwanza wananchi na kweli kabisa mheshimiwa watu awa wanashida sanaa na maisha yao yote walikuwa wanategemea mazao ambayo yanapatikana  kwenye mashamba yao na maamuzi ya kufunga mgodi yamekuja ni baada ya kukasirishwa na majibu ya mgodi” Alisema Mwenyekliti.


Kufuatia malalamiko hayo waziri wa Madini Mh.Stanslaus Nyongo ameunga mkono hatua iliyochukuliwa na wananchi wa Kijiji hicho kwa kufunga barabara inayoingia kwenye Mgodi  kutokana na  kuwepo kwa majibu ambayo yamekuwa yakitolewa ya kukatisha tamaa.

’ Naomba istafsiliwe mlichokifanya ni makosa kufunga au kuzuia njia hii ya kuingia mgodini mmefanya  sawa sawa kwa sababu mnadai haki yenu, nilikuwa namtafuta uyu mzungu toka jana lakini ninataarifa polisi wamemkamata tayari’’ Alisema Nyongo.

Akizungumza na mmoja wa wamiliki wa mgodi Bw ,Alex Kindersley  Naibu waziri  Nyongo amewataka kwa kushilikiana na mkuu wa wilaya ya Geita kumaliza tatizo  hilo ndani ya wiki moja kulipa madai ya wananchi hao tofauti na hivyo kama wizara watachukua  hatua za kinidhamu dhidi ya mgodi .

No comments:

Post a Comment