Monday 4 April 2016

WAZIRI MKUU MSTAAFU WA KENYA MH LAILA ODINGA AMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUMPOKEA CHATO

Waziri mkuu mstaafu wa Kenya mh Raila Amolo Odinga amerejea nchini Kenya baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku 3 huko Lubambangwe katika kijiji cha Mlimani, wilaya ya Chato mkoani Geita, alikomtembelea rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  dkt. John Pombe Magufuli aliyepo mapumzikoni.

Akizungumza katika uwanja wa michezo wa shule ya sekondari Chato kabla ya kuruka kwa helkopta, mh Odinga amemshukuru rafiki yake rais Magufuli kwa kumpokea na pia amewashukuru wananchi wa Chato kwa ukarimu wao kwa wageni.

Mh Odinga pia amesema ana imani kuwa rais Magufuli ataisaidia Tanzania kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo umasikini unaowakabili wananchi wake.

Aidha Odinga na mkewe mama Ida Odinga waliwasili Chato april, 02  2016 kwa mapumziko na kuisalimia familia ya rais Magufuli ambayo ni familia rafiki.

Katika hatua nyingine rais Magufuli ameahidi kutoa madawati na vitabu kwa wanafunzi wa shule 3 za msingi ambazo ni Kalema ,Chato na Kiteta zilizopo wilayani humo, ambao walijitokeza katika uwanja wa sekondari wa Chato, wakati rais akimuaga mgeni wake waziri mkuu mstaafu wa Kenya.



No comments:

Post a Comment