Tuesday 12 April 2016

DAKTARI FEKI AKAMATWA HOSPITALI YA RUFAA MKOANI GEITA

Taasisi ya kuzuia na kupambana na  rushwa (takukuru)  mkoani Geita inamshikilia bw,Shukurani Kulwa Musa,kwa kufanya kazi ya uuguzi bila ya kuwa na sifa ambazo zinamruhusu kufanya kazi hiyo.


Akizungumza na Storm  habari mkuu  wa takukuru  mkoani hapa,Thobias Ndaro, amesema kuwa  taarifa za kupatikana kwa daktari huyo  walizipata wiki moja kabla ya ujio wa waziri mkuu na baada ya kufanya uchunguzi wa kina ulioweza kubaini kuwa bw,Shukurani  hakuwa na sifa za kuwa daktari  hali ambayo ilipelekea kumkamata kwa ajili ya uchunguzi  zaidi.

Ndaro  ameeleza kuwa kwa mjibu  wa uchunguzi  ambao wameufanya walibaini kuwa daktari huyo ni wale watu ambao wanafanya mazoezi ya vitendo na kwamba kwa sasa bado wanaendelea na uchunguzi zaidi na utakapo kamilika watatoa taarifa kamili juu ya daktari huyo.


AidhaStorm habari ilifanikiwa kufika katika ofisi za mkurugenzi na kukutana  na kaimu mkurugenzi wa halamshauri ya wilaya,mwalimu Deus Self,ambapo amesema kuwa ni kweli  alipatiwa taarifa za  mganga huyo ambae ni feki  lakini  kwa madai ambayo mganga huyo alikuwa nayo alidai kuwa anajitolea katika hosptali hiyo.

No comments:

Post a Comment