Thursday 21 April 2016

MTI WAJERUHI WANAFUNZI WAWILI NA KUUA MMOJA WILAYANI BUKOMBE MKOANI GEITA


Wanafunzi watatu wakike wa Shule ya Sekondari Msasa iliyoko  Kata ya Runzewe Mashariki wilayani Bukombe mkoani Geita jana wamepondwa na mti wakiwa Shuleni na  kati yao mmoja amefariki dunia na wenzake wawili kujeruhiwa ambapo wamelazwa  katika kituo  cha afya  cha Uyovu mkoani hapa

 Kwa mujibu wa mkuu wa shule hiyo  Mwl.Mokili Sagama amemtaja aliyefariki Dunia kuwa ni jackline bahati umri miaka 14 kutoka kijiji cha  Nampangwe alikuwa akisoma shuleni hapo kidato cha pili.

Pia amewataja majeruhi wawili kuwa  ni Eva Yohana   kutoka kijiji cha  Msangila  na mwenzake Emiliana Elias kutoka kijiji cha musasa wote ni wanafunzi wa kidato cha pili.


Aidha kamanda wa polisi mkoani  hapa  Mponjoli mwabulambo alisema kuwa ni  kweli jeshi la polisi linatambua kutokea kwa  tukio hilo. 

No comments:

Post a Comment