Thursday 28 April 2016

LUNS HOTEL YANUSURIKA KUUNGUA NA MOTO BAADA YA HITILAFU YA UMEME KUTOKEA KATIKA ENEO LA MITI MIREFU MKOANI GEITA

Hotel ya Luns  iliyopo maeneo ya mtaa wa Miti Mirefu kata ya Kalangalala imenusurika kuungua kwa moto kutokana na hitilafu ya  umeme ambayo ilikuwa imetokea katika nguzo ya mita.

Wakizungumza na Storm habari  baadhi ya mashuhuda waliokuwepo eneo  la tukio wamesema kuwa  hitilafu  iliyotokea katika  hotel hiyo imesababishwa na Transfoma , ambayo imewekwa katika mtaa huo kwani si mara ya kwanza kwakutokea kwa hitilafu  ni mara kwa mara  tatizo limekuwa likijitokeza.

Hata hivyo kwa upande wake,Christina Sunga ambae ni kamanda wa zima moto, amesema  kuwa  taarifa  walizipata kwa wananchi kwa kupigiwa simu na waliweza kufika kwa wakati na kufanikisha kuuzima moto huo.


Kutokana na lawama nyingi kuelekezewa katika shirika la umeme tanesko mkoani hapa,Storm habari imefanikiwa kufika katika ofisi za shirika hilo na kuzungumza na ,mwandisi wa shirika hilo ,Ndemba William,ambapo amesema kuwa chanzo cha moto huo ilikuwa ni hitilafu  ambayo ilianzia katika waya unaoingiza umeme  katika hotel hiyo.

No comments:

Post a Comment