Tuesday 12 April 2016

WAFANYABIASHARA WA SOKO KUU MKOANI GEITA WAJISAIDIA KATIKA MIFUKO NA MAKOPO KWA KUKOSA CHOO

Baadhi ya wafanyabiashara wa soko kuu mkoani Geita wameiomba  serikali kujenga choo katika  soko hilo ili kuondoa kero ikiwemo harufu mbaya inayotokana na  watu kujisaidia katika mifuko na makopo ya maji jambo ambalo linahatarisha afya zao.


Wakizungumza na Storm habari wafanyabiashara hao wamesema serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka juu ya jambo hilo kwani wanalazimika kufanya hivyo kutokana na kukosa choo katika soko hilo na baadae humwanga uchafu huo katika mitaro iliyopo sokoni hapo pindi mvua zinaponyeha.

Katibu wa soko hilo bw, Adriani Rwechungula amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo, huku akidai kuwa jambo hilo linatokana na baadhi ya watu kutokuwa na uelewa juu ya utunzaji wa mazingira ambapo amesema wafanyabiashara wote sokoni hapo wanatakiwa kushirikiana kuweka mazingira safi ili hata wanunuzi wa bidhaa wanapoingia sokoni humo wafurahie huduma zao.

Aidha Storm habari imezungumza na afisa afya wa halmashauri ya mji wa Geita bw, Mabela Ezekiel Mabela ambapo amesema kuwa serikali inafanya utaratibu  wa kutatua jambo hilo huku akiwataka wananchi kutumia choo cha kulipia kilichopo karibu na  maeneo ya soko hilo  wakati serkali iktafuta ufumbuzi wa suala hilo.


Aidha Mabela ametoa wito wa wafanyabiashara wa soko hilo kuacha tabia hiyo mara moja na kwamba yeyote atakaebainika kufanya kitendo hicho serikali haitosita kuchukua hatua kali za kisheria juu yake ikiwepo kufikishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment