Tuesday 26 April 2016

UMOJA WA WAGANGA WA TIBA ASILIA MKOANI GEITA WAMPONGEZA MKUU WA WILAYA YA NYANG'WALE



Umoja wa waganga wa tiba asili wilaya ya Nyang’wale mkoani  Geita umempongeza mkuu  wa wilaya mh  Ibrahim Marwa, kwa kutoa ushirikiano ambao umesaidia kupunguza kasi ya mauwaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi.

Akitoa taarifa hiyo katika mkutano wa waganga wa tiba asilia wilayani humo mwenyekiti wa umoja huo  kanda ya ziwa Bujukano John Mahungu amesema kuwa ushirikiano uliokuwepo kati ya umoja huo na uongozi wa wilaya umefanikisha kupunguza mauaji kutoka asilimia 80% mwaka 2014 hadi kufikia 10% hivi sasa.

Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale mh Ibrahim Marwa ambae alikuwa ni mgeni rasmi katika mkutano huo ,amesema kuwa  kwa  sasa wilaya yake imedhamiria kushirikiana na viongozi wa vijiji kukusanya takwimu za wazee ikiwa ni moja kati ya njia za kudhibiti wimbi  la mauaji.

Aidha Marwa  ameushukuru   uongozi  wa waganga wa tiba  asilia  kwa kutoa elimu kwa waganga waliotoka  maeneo ya vijijini  ikiwa ni pamoja na ulinzi  shirikishi hatua  iliyochangia kwa kiasi  kikubwa kupunguza mauaji katika maeneo yao.

No comments:

Post a Comment