Wednesday 20 April 2016

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MH.MAKONDA ATANGAZA VITA NA WAFANYAKAZI HEWA JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa kazi ya kutafuta watumishi hewa katika manispaa za jiji la Dar es Salaam bado linaendelea baada kubaini njia chafu wanazotumia watumishi hewa hao.

 Akizungumza leo na waandishi habari ,Makonda amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ni kioo kwa nchi hivyo jitihada zinaendelea ya kutafuta na kazi hiyo itafanywa sekta kwa sekta.

Amesema kuwa Wakuu wa Wilaya katika jiji la Dar es Salaam hakuna kufanya kazi yeyote mpaka wamelize kutafuta watumishi hewa kwa kutumia malipo ya watumishi kutoka taasisi za fedha (Pay low).

Makonda amesema idadi ya watumishi hewa 71 aliowasilisha kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –Tamisemi, Georgre Simbachawene  ni ndogo katika  jiji la Dar es Salaam hivyo kazi lazima iwe endelevu.

Amesema kuwa watumishi Hewa hawawezi wakawa wanalipwa mshahara huku wanaofanya kazi kwa moyo mmoja wanajisikia  vibaya hivyo ni lazima watafutwe na wachukuliwe hatua na vyombo vya dola.

Mkuu Mkoa amesema kuwa kati ya watumishi hewa 71 ni watumishi 34 hewa wamefunguliwa mashitaka katika mahakama mbalimbali kutokana kuchukua fedha wasioifanyia kazi.

No comments:

Post a Comment