Saturday 2 April 2016

SERIKALI MKOANI GEITA KUIMARISHA SUALA LA ULINZI NA USALAMA.

Serikali  wilayani Chato mkoani Geita imejipanga kuhakikisha kuwa inaimarisha swala la ulinzi na usalama  kwa kuwatumia  wajumbe wa nyumba kumi.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya hiyo, Shabaani Ntarambe  wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa ulinzi na usalama unaimarishwa watahakikisha kuwa wanawatumia  wajumbe  wa nyumba 10 kwa kuhakikisha kuwa wanaangalia wale wote ambao wanaingia katika  kaya  wanazoziongoza.

Mh.Ntarambe ameongeza kwa kuwataka wananchi kuhakikisha kuwa wanafanyia kazi swala la uhakiki wa silaha zoezi ambalo limeanza jana Aprili 1 na linatarajia kumalizika june 30 mwaka huu.


Aidha amewataka wananchi katika zoezi hilo la kuhakiki silaha kuwa na maelewano kwa wananchi kuwa na hiyari ya kusalimisha silaha zao.

No comments:

Post a Comment