Friday 22 April 2016

SERIKALI KUWEKA MIKAKATI ILI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KATIKA HOSPITALI YA GEITA


Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa inaboresha huduma za afya katika hospitali ya wilaya ya Geita ikiwa ni pamoja na kuipatia  hadhi ya kuwa hospitali   ya mkoa.

Akiuliza swali la nyongeza katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni Dodoma, Mbunge wa Geita mjini Mh.Constatine Kanyasu, alitaka kujua kuwa ni lini watumishi wa afya pamoja na madaktari watapelekwa katika  hosptali  hiyo.

akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Tamisemi, Naibu Waziri Tamisemi Suleman Jafo pamoja na kuwapongeza wabunge wote wa Geita kwa kushirikiana na mgodi wa dhahabu wa (GGM) kwa kazi waliyoifanya amesema kuwa muda si mrefu Wizara ya afya itatoa idadi ya waajiriwa wakati huo hospitali ya wilaya ya Geita ikipewa kipaumbele kwa sababu ina hadhi ya kutosha.


Hata hivyo Mhe.Jaffo amesema kuwa katika bajeti ya mwaka huu Serikali imeweka mikakati mbalimbali katika halmashauri zote nchini ikiwa ni pamoja na kuboresha vituo vya afya, hospitali za wilaya na hospitali za mkoa.

No comments:

Post a Comment