Friday 15 April 2016

JAMII YATAKIWA KUWA NA MTAZAMO TOFAUTI KWA WATU WLIO NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI



Jamii imetakiwa kuwa na mtazamo tofauti kwa watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI  na
kuhakikisha wanaishi kwa furaha bila kunyanyapaliwa na watu
wanaowazunguka.

Hayo yamesemwa na mke wa mtoto wa Mfalme wa norway, mette-marit ambaye
pia ni balozi wa kimataifa wa shirika la umoja la kupambana na UKIMWI na
(UNAIDS) wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu kazi anazozifanya kwa UNAIDS kama balozi ambaye anazunguka maeneo
mbalimbali duniani ili kuelimisha jamii kuhusu UKIMWI.

Mette-Marrit amesema kuwa watu wenye UKIMWI ni kama watu wengine hivyo
wana haki ya kupata huduma bila kunyanyapaliwa ili waweze kuishi kwa
uhuru kama watu wengine na ili kufanikisha hilo ni wajibu wa kila mtu
kuwasaidia waathirika.

Amesema watu kuwa na UKIMWI sio mwisho wa maisha inatakiwa kwanza jamii
kuwa na mtazamo tofauti na inatakiwa kila mtu kusaidia mapambano ya
UKIMWI sio jambo la mtu mmoja mmoja.

Naye mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Dkt.
Fatma Mrisho amesema Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ili
kupambana na ugonjwa huo lakini pia ili kufanikisha mapambano hayo wanahitaji
kushirikiana na Taasisi ambazo zitawasaidia katika mapambano hayo.

Dkt. Mrisho amezitaka Serikali za mitaa kuacha kusubiri mpaka Serikali
ipeleke pesa ndiyo wawasaidie watu wanaoishi na UKIMWI na hivyo waweke
utaratibu wa kutumia sehemu ya mapato yao ili kusaidia mapambano hayo.



Amesisitiza kuwa  Serikali haijalala katika mapambano tunahitaji
kushirikiana na Taasisi ambazo zinatusaidia kupunguza maambukizi mapya
na tunaona Mette-Marit amekuwa akifanya jambo zuri anazunguka sehemu
nyingi ili kusaidia kupunguza maamukizi mapya ya ukimwi.

No comments:

Post a Comment