Tuesday 26 April 2016

WAZAZI MKOANI GEITA WATAKIWA KUWAPELEKA WATOTO KUPATIWA CHANJO

Wazazi mkoani Geita wametakiwa kujenga desturi ya kuhakikisha kuwa wanawapeleka kwenye chanjo watoto walio chini ya umri wa miaka 5 ili kudhibiti magonjwa ya milipuko ambayo yamekuwa yakiwakabili watoto.

Akizungumza katika uzinduzi wa chanjo ya watoto uliofanyikia katika hosptali ya upendo iliyopo kata ya bomba mbili, mwenyekiti wa mtaa wa Mwatulole Charles Fikiri,amesema kuwa chanjo ni muhimu sana kwa watoto ambao wapo chini ya umri wa miaka mitano.

Hata hivyo muuguzi mfawidhi wa  zahanati ya Upendo  Lyidia  Bwanakunu  ameeleza kuwa wamekuwa na wakati mgumu  kutokana na kutoa huduma bure kwa akina mama  wajawazito na watoto hali ambayo imekuwa ikisababisha mlundikano  mkubwa hivyo ameiomba  serikali kuhakikisha kuwa inatoa ushirikiano  ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa .

Kwa upande wake Anastazia Shabani ambae ni moja katika ya wazazi waliofika katika huduma ya chanjo amesema kuwa ni vyema kwa wazazi wengine kuachana na imani ambazo ni potofu  hivyo ni muhimu  kuwaleta  watoto kupatiwa chanjo.


Mkurugenzi wa zahanati hiyo Deogratias  Katunzi ameiomba serikali kutoa msaada wa wauguzi kutokana na kwamba wao wamekuwa wakijitolea kwa kutoa huduma ya afya kwa watoto na akina mama bure kwa   kata mbili.

No comments:

Post a Comment