Monday 18 April 2016

MKURUGENZI WA WILAYA AMSIMAMISHA KAZI MUUGUZI WA HOSPITALI YA RUFAA MKOANI GEITA

toolbox-gloves-np311ws
Kaimu mkurugenzi wa  halmashauri ya wilaya ya Geita Deus  Seif amemsimamisha kazi muuguzi wa hosptali ya rufaa ya mkoa  Fatuma Salumu baada ya kukamatwa akijaribu kutoroka na vifaa tiba vya hosipitalini hapo.


Akizungumza na storm habari kaimu mkurugenzi  huyo, amesema kuwa ameamua kumwandikia barua ya kumsimamisha kazi muuguzi huyo ili kupisha uchunguzi wa jeshi la polisi na kwamba endapo atajulikana hatua kali zitachukuliwa  dhidi  yake.

Seif amewataka watumishi wa halmashauri ya wilaya kuhakikisha kuwa wanazingatia   miiko ya utumishi wa umma kwa kufata misingi na maadili ya kazi.

Fatuma Salumu alikamatwa na mlinzi wa kampuni ya Geita Security Gard akiwa na mipira ya kujikinga na magonjwa mbalimbali wakati wa kutoa huduma za afya maarufu (gloves) mnamo april 15 mwaka huu na baada ya kuhojiwa alidai alikuwa akitaka kuzipeleka katika duka la madawa.



No comments:

Post a Comment