Monday 4 April 2016

GARI AINA YA FUSO LAGONGA NA KUUA MKOANI GEITA


Gari aina ya fuso  yenye namba za usajili T-939bnz  ambalo linafanya kazi za ubebaji wa mawe, limemgonga bw, Emanuel Kang’wena  mwenye  umri wa miaka 26 mkazi  wa Katoro katika njia panda ya kijiji cha Inyara  wilayani na mkoani Geita  na kumsababishia kifo.


Akithibitisha kupokea mwili huo kaimu mganga  mfawidhi  wa kituo cha afya cha Katoro bw,Bahati Machaguli  amesema kuwa  sababu iliyo pelekea kifo chake ni kutokwa na   damu nyingi  eneo  la kichwa


Aidha baadhi ya mashhuda walioshuhudia tukio hilo wameieleza storm habari   kuwa marehemu alitaka kupanda  gari  hilo wakati  likiwa kwenye mwendo  ndipo alipo teleza  na kuangukia katika uvungu  wa gari  hilo na ndipo lilipo mgonga na kufariki  papo hapo 

No comments:

Post a Comment