Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa kumi wa Chama cha Majaji na Mahakimu
wa Jumuiya ya Madola utakaofanyika kuanzia Septemba 25 – 27, mwaka huu jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambali.
Kwa mara ya kwanza Tanzania imepata fursa ya kuwa
mwenyeji wa mkutano wa 10 wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Jumuiya ya Madola
unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 25 – 27 mwaka huu
katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu.
Akizungumuza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar
es Salaam Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim
Hamis Juma amesema kuwa huu utakuwa ni mkutano wa kihistoria kwa Tanzania kwani
ni mara ya kwanza kufanyika tangu kuanzishwa kwa chama hicho.
Alieleza kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano
huo utakaohudhuriwa na wajumbe Zaidi ya 354, unatarajiwa kufunguliwa rasmi na
Makamu wa Rais, Mhesimiwa Samia Suluhu Hassan.
“Mkutano huu
mkubwa katika historia ya nchi yetu ni muhimu sana hasa katika sekta yetu ya
utalii kwani tutapata kutangaza vivutio vyetu vya utalii, tunawaomba wenzetu wa
Wizara ya Maliasili na Utalii kuwepo ili kutangazo sekta ya utalii”, alisema
Prof. Juma.
Akieleza umuhimu wa mkutano huo Prof. Juma alisema
kuwa mkutano huu utawajengea uzoefu na uelewa mkubwa Mahakimu na Majaji wa
mahakama ya Tanzania kwani wapata kujua kuhusiana na masuala ya uhuru wa
mahakama, masuala mikataba ya kimataifa, maendeleo ya kisheria na upatikanaji
wa huduma ya haki.
Aidha Prof. Juma alisema kuwa kati ya washiriki
kutoka Tanzania watapata uzoefu wa sheria katika maeneo mageni kama sheria mpya
za kushughulika na magaidi duniani na mitandao ambapo uvunjwaji wa sheria
umekuwa mkubwa sana.
“Kwetu Tanzania mkutano huu ni muhimu sana kwa
sababu majaji na mahakimu wetu wapatao 50 ambao watahudhuria watapata fursa ya
kujengewa uwezo na kubadilishana uzoefu na wale wanaohudhuria hasa kwa maeneo
ambayo ni mapya kwa mfano jinai za kigaidi, makosa ya kimutandao ni maeneo
ambayo yahitaji uzoefu wa kutosha”, alieleza.
Aidha Prof. Juma alisema kuwa mada mbalimabli
zitatolewa katika mkutano huo kama kukabiliana na vizuizi katika upatikanaji wa
haki, rushwa, utovu wa maadili pamoja na uendeshwaji wa kesi katika maeneo
mapya kama ughaidi na makosa ya kimutandao huku Tanzania wakipewa kuwasilisha mada katika maeneo ya ujangili na uboreshaji
wa upatikanaji wa haki mahakamani.
Tanzania ni mwanachama halali wa Chama Majaji na
Mahakimu kutoka nchi za Jumuiya ya Madola tangu mwaka 1970 huku mkutano huo
ukifanyika kwa mara ya kwanza kwa Tanzania.Mara ya mwisho mkutano huo
ulifanyika Guyana, Amerika ya kusini ambapo mahakama ya Tanzania ilituma wawakilishi
wake.
No comments:
Post a Comment