Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akisalimiana na baadhi ya
Viongozi wanaosimamia Uwanja wa Nangwanda Mtwara wakati alipofanya ziara
kujionea changamoto katika uwanja huo 25 Septemba, 2017 Mkoani Mtwara.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akiongea na baadhi ya
Viongozi wanaosimamia Uwanja wa Nangwanda Mtwara wakati alipofanya ziara
kujionea changamoto katika uwanja huo 25 Septemba, 2017 Mkoani Mtwara.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akiangalia eneo la uwanja wa mpira
wa miguu akiwa na baadhi ya Viongozi wanaosimamia Uwanja wa Nangwanda Mtwara
wakati alipofanya ziara kujionea changamoto katika uwanja huo 25 Septemba, 2017
Mkoani Mtwara.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kwamba pindi
Uwanja wa Taifa Dar es Salaam utakapokamilia kufanyiwa ukarabati atahakikisha
anapatikana Mkandarasi Mpya mwenye vigezo na ambaye ataleta mabadiliko hususani
katika utoaji tiketi kulingana na namba za viti vilivyopo ndani ya Uwanja huo.
Kauli hiyo ameitoa
jana Mkoani Mtwara wakati alipotembelea Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Nangwanda
ili kujionea miundombinu ya uwanja huo ikiwemo baadhi ya changamoto
zinazoikabili kiwanja hicho.
Dkt. Mwakyembe
ameeleza kwamba, kumekuwa na changamoto ya kutofahamika idadi kamili ya watu
wanaoingia ndani ya uwanja hali inayopelekea watu kukaa ovyo katika sehemu
zisizo rasmi na wengine kulundikana nje ya uwanja wakati pesa za viingilio
wamelipia ambapo ameweka wazi kuwa hali hiyo inasababishwa na urataibu mbovu wa
utoaji tiketi.
Akiongea na Uongozi wa
Uwanja huo wa Nangwanda Mkoani hapo alisema kwamba, kwakuwa sasa Uwanja wa
Taifa uko katika ukarabati, pindi utakapokamilika Mkandarasi mpya lazima apatikane
ili pindi mtu anunuapo tiketi yake iendane na kiti chake atakachokaa na sio
vinginevyo kwakuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kuboresha sura za viwanja
nchini.
“Napenda kusisitiza
suala hili kuwa, ntahitaji apatikane Mkandarasi atakaetoa tiketi kulingana na
siti atakayokaa mtazamaji wa mpira, kwasababu kumekuwa na kero kubwa katika
utoaji tiketi hapo mwanzo jambo ambalo halileti sura nzuri kwa jamii”, alisema
Dkt. Mwakyembe.
Aliongeza kuwa
Watanzania hawanabudi kuiga mifano ya nchi nyingine ambazo zimejidhatiti katika
masuala ya utoaji tiketi wakati wa michezo.
Sambamba na hayo,
Waziri Mwakyembe ameupongeza uongozi wa uwanja huo kwa kazi kubwa wanayoifanya
ya kuutunza uwanja wa Nangwanda huku akiaihidi kuzifikisha changamoto za uwanja
huo katika Viongozi wa Juu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ili waweze kushirikiana
kwa pamoja kuona namna ya kuzitatua.
Uwanja wa Nagwanda
ulianzishwa miaka ya 1980 ambapo awali ulikuwa ukiitwa jina la Uwanja wa Umoja
Mtwara na baadaye kupewa jina la Uwanja wa Nagwanda lililotokana na jina la mtu
maarufu wakati huo.
No comments:
Post a Comment