Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati)
akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu
sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bibi. Albinus Chuwa na kulia ni Mjumbe kutoka Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Raynold Mfungahema
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bibi. Albinus Chuwa (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
Mwakilishi
kutoka kampuni ya IPSOS inayokusanya takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji Bw.
Samuel Muthoka akiwasilisha taarifa ya namna kampuni hiyo inavyofanya kazi
wakati wa kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu
sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
kutoka African Swahili Televisheni
akichangia mada wakati wa kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa
takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (waliokaa watatu
kulia) katika picha ya pamoja na wadau walioshiriki kikao cha wadau wa
ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji jana Jijini
Dar es Salaam. Watatu kushoto waliokaa ni Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) Bibi. Albinus Chuwa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.
Harrison Mwakyembe amepiga marufuku matumizi ya takwimu zinazotolewa na kampuni
ya GeoPoll zinazohusu Kiwango cha wananchi kusikiliza na kutazama vituo vya
Redio na Televisheni hapa nchini kwa kuwa takwimu hizo zina mapungufu makubwa.
Waziri Mwakyembe alitoa agizo hilo jana jijini Dar
es Salaam baada ya kukutana na makampuni ya ukusanyaji na usambazi wa takwimu
kwa upande mmoja na watumiaji wa takwimu ambao ni vituo vya Redio na
Televisheni kwa upande mwingine.
Katika kikao hicho cha pamoja, makampuni ya IPSOS
Tanzania, Push Observer na GeoPoll walifafanya mawasilisho ya namna
wanavyokusanya takwimu wakati Ofisi ya Taifa ya Takwimu yenyewe ilifanya
wasilisho la kuonesha njia bora na sahihi za ukusanyaji na usambazaji takwimu.
Hata hivyo kamapuni ya Geopoll haikuhudhuria kikao hicho.
“Nimeamua kuzuia utumiaji na usambazaji wa takwimu
za kampuni ya GeoPoll hapa nchini baada ya kugundua tafiti za hii kampuni zina
mapungufu makubwa na kusababisha malalamiko mengi kutoka kwa wadau na wamiliki
wa vituo mbalimbali vya radio na televisheni,” alieleza Waziri.
Kutokana na kupigwa marufuku matumizi ya takwimu za
GeoPoll nchini, Waziri pia ameyataka makampuni yanayofanya uwakala wa kusambaza
matangazo katika vituo vya Televisioni na Redio kusitisha kutumia takwimu za
kampuni hiyo kama kigezo cha kutoa matangazo kwa vituo vya Televisheni na
Redio.
Aidha Dkt. Mwakyembe alifafanua kuwa kama nchi haiwezi
kwenda kwa utaratibu huu, kwani dunia ya leo ni ya biashara na ushindani ni
mkubwa ambao unaendana na kujiuza na kujitangaza kwa chombo husika, hivyo
alihoji “utajiuzaje kwenye soko kama watu wanaotakiwa kubeba matangazo yako
wanatoa taarifa zinazosema kuwa wewe ni mdogo wakati ni mkubwa?.”
Dkt. Mwakyembe ameunda kamati ya watu watatu
inayohusisha Idara ya Habari (MAELEZO), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambayo itafanyia kazi maoni yaliyotolewa
na wadau katika kikao hicho na na mwishoni mwa mwezi wa kumi iwasilishe
mapendekezo ya namna bora ya ukusanyaji na usambazaji takwimu kwa mujibu wa
sharia na taratibu.
Mmoja wa wachangiaji katika kikao Bi. Basilisa
Biseko kutoka vituo vya Radio na
Televisheni alishauri Serikali iweke viwango vya namna ya kufanya utafiti wa
takwimu ambavyo vitatumika na makampuni yote ya takwimu, lengo likiwa ni
kuondoa udanganyifu na kutofautiana katika taarifa mbalimbali za idadi ya
wasilikilizaji wa radio na watazamaji wa runinga.
Mweji Julai mwaka huu Ofisi ya Taifa ya Takwimu
iliizuia kampuni ya Geopoll yenye makao yake makuu nchini Kenya kufanya tafiti
za usikilizaji na utazamaji wa Redio na Televisheni kwa sababu utafiti zao
kushindwa kukidhi vigezo na masharti ya ufanyaji tafiti hapa nchini.
No comments:
Post a Comment