Baadhi ya vikundi vya
wajasiriamali wakifuatilia Semina ambayo ilikuwa inafanyika katika ukumbi wa
halmashauri ya Mji wa Geita.
Kikundi cha wasaniii ambacho
kinajihusisha na shughuli za ujasiriamali kikifuatilia semina.
Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima TCCIA Mkoani Geita
kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Nchini (TRA) imewakutanisha
wafanyabiashara wadogo na wakubwa kwa lengo la kuwapatia
elimu ambayo itawasaidia kulipa kodi.
Akizungumza na wafanyabiashara hao ambao walikuwa wamejitokeza kwenye
ukumbi wa halmashauri ya Mji wa Geita,Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya
ya Geite ,Mwl Herman Kapufi ,amesema wajasiriamali wanatakiwa
kusajiliwa na kujua elimu ya mlipa kodi ambayo itawasaidia kujulikana na
kutambulika serikalini.
Akizungumza na Stormfm Meneja wa TRA Mkoani Geita, James Jilala amesema
kwa mujibu wa mabadiliko ya sheria za
nchi wafanyabiashara ambao wanakuwa sio rasmi wanatakiwa kuwa
kwenye vikundi maalum ambavyo vitatambuliwa na kupatiwa elimu ambayo
itawasaidia kuwa walipa kodi wazuri.
Katibu wa TCCIA Mkoani Humo,Mariam Mkaka ameelezea kukosekana
elimu ya ujasiriamali ni chanzo ambacho kimekuwa kikisababisha vikundi vingi
kutokusimama na kujikuta vinaanguka.
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo ambao wameshiriki
katika semina hiyo, Rose Michael ,Jackson Mlenga na Winfrida Marius wameeleza
kuwa semina hiyo itawasaidia kupata Elimu ya ulipaji Kodi.
No comments:
Post a Comment