Mwenyekiti
na mjumne wa kamati ya maandalizi ya tamasha
la 11 la Wanawake Wajasiriamali(MOWE) Bi.Anna Matinde akieleza jambo kwa
waandishi wa habari(hawapo pichani) kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wajasiriamali
Bi.Zubeda Lous na kushoto ni mjumbe wa Umoja huo wakati wa utambulisho wa
tamasha na semina kubwa ya 11 litakalofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam
kuanzia tarehe 24-30 oktoba ,2017 utambulisho huo ulifanyika hivi leo katika
ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Umoja wa Wanawake Wajasiriamali (MOWE)
Bi.Zubeda Sembo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
kushoto ni Katibu wa Umoja huo Bi. Naomi Kamba na kutoka kulia ni mjumbe wa
MOWE wakati wa utambulisho wa tamasha na semina kubwa ya 11 litakalofanyika
viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaa kuanzia tarehe 24-30 oktoba ,2017 utambulisho
huo ulifanyika hivi leo katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es
Salaam.
Umoja wa wanawake wajasiriamali (MOWE) wameandaa tamasha la 11 kwa wajasiriamali litakalofanyika kuanzia tarehe 24-30 oktoba , 2017 katika viwanja wa mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam lengo ikiwa ni kupanua wigo wa masoko pamoja na kuonyesha bidhaa na fursa mbalimbali za kijasiriamali zinazopatikana hapa nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati ya
tamasha hilo, Bi. Zubeda Kiluwa amesema kuwa, tamasha hilo litakuwa na kauli
mbiu isemayo‘Mwanamke mjasiriamali funguka shiriki kujenga Tanzania ya viwanda’
“Tunawaalika
wanawake wote popote walipo kushiriki maadhimisho na maonyesho haya kwani
yatawahusiha wadau mbalimbali wa maendeleo ya wanawake, Wizara pamoja na
taasisi za serikali na mashirika binafsi,”alisema Kiluwa.
Tamasha
hilo litafunguliwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.
Charles Mwaijage ambapo wadau watakaoshiriki kutoa elimu za kijasiriamali
katika tamasha hilo ni pamoja na Wakala wa Usajili Biashara na utoaji
leseni (BRELA), TRA, GSM, SIDO, TBS, TFDA pamoja na wawakilishi kutoka
katika benki mbalimbali ambao kupitia semina hiyo watatoa elimu juu
ya ujasiriamali.
Aidha
Bi.kiluwa ameleza kuwa gharama zitakazotozwa kwa wajasiriamali watakaoshiriki
katika maadhimisho hayo ni shillingi 50,000 kila mmoja, na kwa yeyote
atakayeshiriki kwaajili ya uzinduzi, ununuzi na kujionea bidhaa mbalimbali
hawatatozwa gharama yoyote.
Kwa
upande wake mjumbe wa kamati ya tamasha hilo Bi.Anna Matinde amaesema kuwa
tamasha hilo halitawahusisha wajasiriamali peke yake bali litawahusisha watu
wote lengo likiwa ni kubadilishana mawazo ya kimaendeleo katika kuunga mkono
sera ya Tanzania ya viwanda.
“Tanzania
itajengwa na watu wengi, kupitiwa mawazo ya wajasiriamali na wale wasio
wajasiriamali watapata kujua mambo mbalimbali juu ya elimu ya ujasiriamali,
namna ya kujiajiri na kuondokana na wimbi la ukosefu wa ajira,” alifafanua Bi.
Matinde.
Aidha Bi. Matinde
amefafanua kuwa tamasha hilo halitowahusisha wanawake pekeyake bali hata
wanaume wenye fursa mbalimbali za ujasiriamali wanakaribishwa kutangaza
kazi zao na kujipatia elimu itakayotolewa .
No comments:
Post a Comment